GET /api/v0.1/hansard/entries/697873/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 697873,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/697873/?format=api",
"text_counter": 284,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Muthama",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 96,
"legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
"slug": "johnson-muthama"
},
"content": "Bw. Spika wa Mda, nakanyanga zulia, yule mtoto ninayewakilisha na ninasema ninapokula kiapo cha mwenyezi Mungu, asilimia 10 ya watu wa Machakos, watoto ambao wazazi wao walinituma hapa wanasomea chini ya miti. Kuwe jua au mvua, anapata taabu pale. Ni ile ile serikali iliyonipatia hili zulia imeniwekea maji hapa. Yule mtoto ninayemwakikilisha na mamake amenituma hapa nimsaidie nimtoe kwenye ugandamizaji wa umaskini na utumwa, bado mtoto wake hana mahali pa kuenda. Pia, ni hii serikali inayoenda kukopa Ksh400 bilioni kujenga reli ambayo itatumiwa na mabepari kwa sababu asilimia 10 ya watoto hao masikini ambao hawatapata elimu – tuseme ukweli – watawezaje kujimudu kufikia kiwango cha kutumia hii reli isipokuwa tu inajengewa watu wa nje waje hapa ili waendelee kutunyonya wakitumia na kuandika watu wetu. Yule mtu anayepata mshashara wa elfu Kshs12,000 anaandikwa na bepari. Bepari anakuja hapa na kusema nimewapa watoto wenu kazi lakini anapata ujira wa Kshs12,000. Anafanyia mkate wa kila siku na wakati ataacha kazi hiyo, atakuwa mwombaji na maskini. Ni hiyo hiyo serikali ambayo inashindwa kujenga madarasa ya watoto wetu kusomea; ni hiyo hiyo serikali ambayo Rais akiingia katika barabara, msafara wa magari yake haupungui magari 20; ni hiyo hiyo serikali ambayo Naibu wa Rais akitembea anaenda na helikopta tatu zinapaa kwenye anga akiangalia maskini wakiwa chini akitumia pesa za Serikali halafu hii ripoti imeandikwa kutoka nje katika kujaribu kutatua shida zetu ni kama hao watu wanaishi na sisi. Bw. Spika wa Mda, ikiwa tutajimudu na kufika pahali, lazima sisi kama taifa tuwe Wakenya, tufikirie kama Wakenya na tuangalie masilahi yetu na kuona ni nini tutapatia kipao mbele. Bw. Spika wa Muda, mimi najua Mwenyekiti ameileta repoti hii mblele ya Bunge hili. Lakini ripoti itawezaje kumfikia Mhe. Rais Uhuru Kenyatta ndio ajuaye kwamba kazi anayowafanyia wananchi, hasa katika sekta ya elimu, ni duni sana. Ripoti hii inamlenga yeye. Nikiisoma na mwuona Mhe. Rais wa Kenya. Serikali hii sasa inasema ya kwamba itatoa mitambo ya lapto kwa watoto wetu. Wanatumia mabilioni ya pesa kununua mitambo hii na inapeleka katika shule ambazo hazina stima au madarasa. Hata kama mitambo hii itatumia nguvu za jua au solar system, watoto hawawezi kusomea nje kwa sababu jua ni kali sana. Sasa huyo mtoto anapewa mzigo mara mbili; kwanza, hawezi kusoma. Mzigo wa pili, ni kubeba mitambo hiyo na wa tatu haelewi ni mtambo ya aina gani. anatumia. Serikali hii ina wasomi ambao Mungu amewapa kipawa cha kuweza kusaidia yule anastahili kusaidiwa. Hata hivyo, wanaenda mbele huko wakirudi nyuma katika mambo haya ya elimu. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}