GET /api/v0.1/hansard/entries/697875/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 697875,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/697875/?format=api",
    "text_counter": 286,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Bw. Spika wa Muda, kama tungefika pahali tungeacha yale mambo yanafanyika leo. Ukiangalia leo, Serikali ya Jubilee inatumia kiasi kikubwa cha pesa ya nchi kutembea kila pahali. Juzi Mhe. Rais alizuru Mombasa kwenda kumpatia Mhe. Mwahima bahasha iliyojaa pesa. Alibeba namna hii. Alipewa kibunda cha pesa. Halafu inaonyeshwa kwa televisheni niaking’ang’ana kuiweka katika soksi zake na mifuko ya koti lake. Ni aibu kuona watoto kutoka sehemu yake hawana madarasa ya kusomea. Mungu awe na huruma kwa nchi hii. Leo tunatumia hizo pesa kufanya kampeni.Matatizo yetu sasa ni kwamba kuna Mhe. Rais wa sasa na kuna Mhe. Rais wa mwaka 2022 mpaka 2032. Hizo pesa zinatoka wapi? Mhe. Rotich ambaye ni Waziri wa Fedha, hajatenga pesa hizi za kaimpeini. Hakuna kuficha; pesa hizi ni za Shirika la Huduma yaVijana hapa nchini. Kama tungekuwa Merikani au Uingereza, kwa sababu ufisadi huu, Mhe. Rais hangejiuzulu na kumwachia mtu mwingine mamlaka. Ikiwa mkuu wa kitengo cha Upelelezi anaweza kukaa mbele ya Kamati ya Bunge na kusema kwamba yule mtu alistahili kuchunguza pesa zilizoibiwa, aliungana na wale wezi, basi angefutwa kazi mara moja. Ameaandikiwa barua ya kwanza acha kazi na bado yuko kazini. Ya tatu, ya nne, ya tano na ya sita na bado yuko kazini. Mtu huyo bado anafanya kazi ndani ya Serikali ya Mhe. Uhuru Kenyatta na ana cheo cha juu sana. Mhe. Rais Kenyatta yuko bado kitini. Jambo la pili, Mkuu wa Kitengo cha Upelelezi anasema kwamba eti ukipata zabuni ya Kshs2 milioni, kazi yako ili kuwa rahisi sana kuongezea sufuri mbele yake. Sufuri tu mbele yake. |Kwa mfano, Ksh2.4 milioni ukiongezea sufuri tu, inakuwa Ksh24 milioni. Lakini Local Purchase Order (LPO) yenyewe ile ya kutoa huduma ya kupewa hiyo sababu ya kulipa hiyo pesa inasema Ksh--- Naona kama wakati wangu umeisha."
}