GET /api/v0.1/hansard/entries/698295/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 698295,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/698295/?format=api",
    "text_counter": 162,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Bady",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1612,
        "legal_name": "Bady Twalib Bady",
        "slug": "bady-twalib-bady"
    },
    "content": "Asante sana, Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii ili nami nichangie Mswada huu. Kwanza, ningependa kushukuru Mswada huu kutoka Bunge la Seneti. Ni Mswada mzuri kwa sababu watoto wengi hukosa elimu kwa sababu ya kukosa msingi bora. Niseme kwamba tumeanza kuona matunda ya Mswada huu. Kwa mfano, pale Jomvu, eneo Bunge langu, ipo shule ya msingi ya Jomvu ambayo inayo shule ya chekechea. Mheshimiwa Ali Hassan Joho, Gavana wa Mombasa, aliona umuhimu kuhakikisha kwamba shule za chekechea zina ufanisi na zinajengwa kwa muundo wa kileo. Ninayo imani kwamba haya anayofanya Gavana Joho atayafanya vile vile katika nchi nzima kwa maana tunamtarajia kuwa rais wetu katika siku zijazo. Ni muhimu Serikali itoe pesa kwa wingi kugharamia shule hizi za chekechea ili wazazi wasitozwe ada kubwa. Ni muhimu kwa Serikali kutuma pesa kwa wingi ili wazazi wasilipe kwa sababu tunaona watu wengi hulipa pesa za Parents Teachers Association (PTA) kuwezesha malipo ya walimu hawa. Pia, ni muhimu kwa Serikali kuona kuwa tunafanya juhudu kutuma pesa hizi kwa kaunti ili walimu wa chekechea waandikwe kwa wingi ili kukimu mahitaji ya idadi ya watoto ambao wanaingia katika shule hizo za chekechea. Mswada huu wa Elimu ya Chekechea kwa Kaunti ni mzuri kwa sababu zamani watoto wengi katika misingi yao ya kuanza kusoma, walisomea chini ya miti. Wengine wanasomea katika majumba ya matope. Kuja kwa Mswada huu kutaonyesha msingi bora kwa kuwa watoto wanatakikana kuwa na msingi dhabiti kwa safari yao katika elimu."
}