GET /api/v0.1/hansard/entries/698298/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 698298,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/698298/?format=api",
"text_counter": 165,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Bady",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 1612,
"legal_name": "Bady Twalib Bady",
"slug": "bady-twalib-bady"
},
"content": "Nikiwa Mbunge wa Jomvu, nimeupongeza sana Mswada huu. Nimeupongeza kwa ajili ya kunifaidi katika eneo Bunge langu. Shule ya chekechea ambayo imejengwa, watoto wataendelea kusoma na wataonekana kwa fikra zao kuwa wanasomea mahali ambapo ni pazuri. Mswada huu umezungumza kuhusu shahada ya diploma kwa wale watasomesha shule za chekechea. Tumeona kuwa watu wengi wamesoma kozi za elimu ya msingi ya watoto katika vyuo tofauti tofauti. Ni jukumu letu sasa kuangalia katika serikali za kaunti na Serikali Kuu tuone kuna mpango mzuri ili walimu waandikwe kwa wingi na watoto wetu wapate elimu hii. Kwa hayo machache, Mswada huu umenifurahisha. Ninaona watoto wetu watakuwa na elimu bora na sio bora elimu. Asante na Mwenyezi Mungu atubariki."
}