GET /api/v0.1/hansard/entries/698300/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 698300,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/698300/?format=api",
    "text_counter": 167,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda. Nami pia nataka kupongeza Maseneta kwa kutuletea Mswada huu kuhusu shule za chekechea. Shule za chekechea zilikuwa zikichukuliwa kiholela holela hapa nchini. Mpaka mfumo wa ugatuzi ulivyokuja, shule za chekechea zikawa zikiangaliwa kama shule ambazo zina umuhimu. Mswada huu wa kutengeneza sheria ya kuwezesha shule za chekechea kujenga msingi bora kwa elimu yetu hapa nchini ni mzuri. Tukipitisha sheria hii, itawawezesha watoto wetu kuwa na mwanzo kamili ulio na msingi mzuri ili waweze kuendelea mbele. Isipokuwa watoto wetu walio shule za mjini waliokuwa wakipata elimu bora ya chekechea, Wakenya wengi kule mashinani hawakupata msingi huu. Yeyote yule aliyemaliza shule ya upili ama hata hakuendelea na kumalizia shule ya upili alijitolea kufunza hawa watoto. Kisa na maana ni kuwa Serikali haikutilia maanani elimu hii wakati ule. Sasa hivi, kuna vyuo vingi, hata vyuo vikuu, ambavyo vinasomesha watu kuhusu masuala ya shahada za shule za chekechea. Hivyo basi, sheria hii ikiwa itapita, na nina imani itapita, watoto wetu watapatiwa elimu iliyo bora ili wawe wamepewa msingi unaofaa wakianza maisha ya kielimu. Wakati NG-CDF ilianzishwa ndio wakati shule hizi za chekechea zilianza kujengwa na kupewa majengo yanayostahili kwa watoto wetu kosomea na vile vile, kupatiwa madawati ili waweze kusoma. Juu ya hapo na kwa sababu walimu walikuwa hawapatiwi mshahara unaofaa, ni wazazi walitoa hela zao kidogo kuwawezesha wale walimu kuja shuleni kila siku kuwafunza hawa watoto. Hivyo basi, ilikuwa shida sana kwa watoto hawa kufunzwa inavyostahili. Hivi sasa, bila hata hii sheria kuanza kufanya kazi, tayari tumeona mabadiliko makuu. Hii ni kuanzia kuja kwa NG-CDF na ugatuzi. Hii ni pamoja na shule hizi za chekechea kuwekwa chini ya himaya ya Magavana nchini. Tumeona tofauti kubwa sana. Bila shaka, walimu hawa waliosomea shahada hii ya kusomesha watoto wetu wanaweza kupatia watoto msingi unaofaa sasa hivi. Katika Kenya nzima tukisema kuwa tutatumia shahada ya stashahada ili kuwaandika walimu, haitawezekana kwa sababu kuna viwango tofauti vya kusomea mafunzo ya kusomesha watoto wa chekechea. Kuna shahada ya kwanza ambayo ni cheti, ya pili ni stashahada na ya tatu ni shahada kutoka chuo kikuu. Hapo, nafikiria Kamati ya Elimu, Utafiti na Teknolojia itawezesha Bunge hili kufahamu ya kwamba kuna umuhimu wa wale ambao wako na cheti kufunza kwenye shule za chekechea maanake pia wao wamepewa mafunzo yanayofaa kuwafunza watoto na tumeona tofauti kubwa sana. Napongeza wenzangu kwa vile wamefahamu umuhimu wa kuwa na sheria ya kufanya mipangilio inayofaa kwenye elimu yetu ya chekechea. Si tu kuwa na madarasa peke yake. Kama tunavyosema, watoto wale ni wadogo na wanahitaji kuwa na uwanja wa kuchezea na wa kuwekewa vifaa vya kuwachezesha ili, katika hali ya michezo, wawe kama watoto wengine. Wasiwe ni darasa peke yake bila kuwa na vifaa vya kufanya michezo. Mhe. Naibu Spika wa Muda, tunavyosema, unamuwahi mtoto awali ili aweze kujenga kimaisha, haswa kwenye elimu, ili apate elimu inayofaa ndio aweze kuendelea mbele. Nami pia, naunga mkono."
}