GET /api/v0.1/hansard/entries/698339/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 698339,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/698339/?format=api",
"text_counter": 206,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika wa Muda, kwa kunipa nafasi kuzungumzia Mswada huu ambao unazungumzia taratibu za shule za chekechea. Masomo ya shule za chekechea ndiyo nguzo ya masomo katika zile ngazi zote mpaka chuo kikuu. Kwa muda mrefu sana, nchi yetu ilikuwa imepuuza masomo hayo ya chekechea. Hivyo basi, watoto wengi wamekosa kupata masomo ya chekechea. Ni muhimu sana na nimefurahi kwamba Mswada huu unazungumzia miundo misingi ya kuwezesha kuwepo, katika hii Jamuhuri yetu ya Kenya, shule za chekechea. Ingekuwa vizuri zaidi iwapo tunajenga shule mpya, tujenge hapo hapo shule ya chekechea, shule ya msingi na shule ya upili. Tukifanya hivyo, tunawapatia fikra watoto wetu kwamba masomo ni mtiririko wa ngazi fulani mpaka kufikia ngazi fulani. Hivyo basi, tutaweza kuzuia watoto wengi kuacha shule katika chekechea ama katika shule ya msingi bila kuendelea hadi chuo kikuu. Nashukuru kuletwa kwa Mswada huu kwa sababu unazungumzia elimu bora. Utatuwezesha kuhakikisha kwamba elimu inayopeanwa katika shule za chekechea inaambatana na ratiba ya kitaifa. Kuna shule nyingi za chekechea ambazo zimefunguliwa na watu binafsi. Ukipitia katika shule zile, unapata kwamba yale masomo yanayosomeshwa hapo ni tofauti sana na masomo katika shule za chekechea za umma. Tatizo hapa ni kwamba watoto wetu wanakuwa na mbinu tofauti za kielimu. Kunatokea mtafaruku katika mitaala ama “syllabus” katika lugha ya Kiingereza. Tunapozungumzia hili suala la shule za chekechea, tunatakikana tufikirie zile sehemu kame - yaani sehemu za wafugaji ambazo zina umaskini sana. Sharti tuweke mipango ya chakula hata kama ni kuwapa watoto vitafunio. Wakati wanapopumzika shuleni, wapatiwe angalau chakula kidogo ili waweze kuhimili hali ngumu. Tunatakikana kuwa na takwimu ili tujue shule za chekechea ni ngapi. Utapata katika eneo Bunge fulani, kuna zaidi ya shule za msingi 20, lakini shule za chekechea labda ni tano ama sita. Sijui ni hesabu gani ambayo itawezesha wale watoto wa chekechea waweze kupanda hadi daraja la pili la elimu. Kwa hivyo, tunapojenga shule za msingi, basi tujenge shule za chekechea sambamba ili hesabu iwe sawa. Vile vile, nimefurahi kwamba kutakuwa na ushirikiano wa Serikali kuu, serikali ya kaunti na watu binafsi ambao wanajenga shule za chekechea. Ninayo furaha kwa sababu Mswada huu unapendekeza kushirikishwa kwa washikadau wengine. Hili ni suala ambalo lazima litiliwe uzito. Waswahili wanasema: “Samaki mkunje angali mbichi.” Lazima watoto wetu tuwafunze maadili mema katika shule za chekechea ndiposa waweze kuwa na maadili mema. Kwa sababu sasa tuna ugatuzi, lazima Serikali za ugatuzi katika kaunti zetu ziweze kuongeza bajeti ili shule nyingi za chekechea zijengwe na hata kuboresha zile ambazo ziko. Zile ziliopo zinatupatia masikitiko sana. Nyingine watoto wanasoma kwenye uwanja. Wanapata maradhi na hata funza. Tumezungumzia katika Mswada huu kuwa elimu hii ya chekechea iwe lazima na bure. Pindi tunapopitisha mambo kama haya, lazima tuhakikishe kwamba hata yule aliye chini kabisa kwa mfano katika sehemu ya North Horr--- Hayo maeneo yana ukame na shida nyingi. Kwa hivyo, sharti tuweke miundo misingi ambayo itahakikisha kwamba walimu watapatikana na vifaa vinavyohusika vitapatikana ili watoto hao waweze kupata masomo mazuri. Mafunzo ya walimu wetu wa shule za chekechea lazima tuyapige darubini. Kuna taasisi nyingi ambazo zinafundisha watu elimu ya chekechea lakini utakuta zina tofauti. Nyingine ziko pale kwa kujibinafsisha ama kwa sababu ya kujipatia pesa. Unapata wengine wanaambiwa watahitimu baada ya miezi mitatu ama miezi sita ama mwaka moja. Inakuwa hakuna kanuni ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}