GET /api/v0.1/hansard/entries/698340/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 698340,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/698340/?format=api",
"text_counter": 207,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "kitaifa inayoshikilia kwamba ili mtu afuzu kutoka taasisi ya kuwafunza walimu wa shule za chekechea, sharti awe amesoma kwa muda fulani ndiposa apate shahada. Kwa hivyo, mikakati hii lazima tuiangalie ndiyo tujue kwamba watoto wetu watapata mafunzo yaliyosawia na kanuni zetu. Tukifanya hivyo, tutaboresha elimu ya watoto wetu. Vilevile, lazima tuwaangalie watoto ambao wana ulemavu. Ama kwa kweli, sisi kama Wakenya hapa tumeanguka mtihani. Hii ni kwa sababu hata katika shule zetu za msingi, bado hatuna miundo misingi ya kuwawezesha watoto walemavu kupata elimu bora kama wale watoto wasio na ulemavu wowote. Kwa hivyo, ni lazima serikali za kaunti - kwa sababu tumeambiwa tumefanyiwa ugatuzi - zishirikiane na Serikali kuu katika kushughulikia watoto walemavu. Hao ni watoto wetu pia na lazima wapatiwe haki zao. Zile shughuli ambazo tunaona ni za kimsingi kwa mfano kuhamasisha, kueneza na kutoa habari kuhusu masuala ya shule za chekechea, lazima tuzifanye. Nakubaliana na Mswada huu kwa sababu umezungumzia mambo haya yote. Mswada huu pia umezungumzia suala la ukaguzi wa kijamii katika kuangalia matakwa ya shule za chekechea. Hili litatuwezesha kujua takwimu kuhusu asilimia ya watoto ambao wanapaswa kuhudhuria masomo katika shule za chekechea. Tukiangalia, watoto wengi wanakaa nyumbani na kwenda tu kuanza darasa la kwanza. Inakuwa vigumu kwa mtoto kama huyo kufanya vizuri darasani kwa sababu atakuwa amekosa nguzo ambayo ingemwezesha kuwasiliana na mwalimu kwa njia rahisi akiwa kidato cha kwanza. Vile vile, ili shule hizi ziendeshwe vizuri na kuwe na utekelezaji kulingana na kanuni na sheria, ni lazima kuwe na bodi ya utekelezaji. Tusichukulie kuwa hii ni elimu ndogo kwa sababu tunasema kuwa kila kitu ni lazima kiwe na nguzo. Ni lazima tuwe na bodi ambayo itaangalia shughuli zote husika na kuboresha elimu hiyo. Serikali za kaunti sharti zichukue hatamu na kubidiika kuonyesha kwamba hili ni jambo muhimu. Ni sharti waweke mikakati zaidi ya kuboresha elimu ya chekechea. Tukiangalia usalama wa watoto wetu, ni masikitiko makubwa kuwa kuna pahali ambapo shule za chekechea zimejengwa karibu au pembezoni za barabara na hakuna vigezo vyovyote vya kuwasaidia watoto wale kupita huko. Hayo ni matatizo makubwa. Kiafya, chekechea nyingi hazina sehemu za kujisaidia ama kupumzika wala watoto kujivinjari kimichezo. Katika elimu, vitu hivi ni msingi na tusiache kwa kusema kuwa ni vitu vidogo. Majanga hutokea na ni muhimu tujue vigezo ambavyo vitasaidia kukitokea moto, na kuhakikisha kwamba watoto watakuwa salama. Mhe. Spika, najua wenzangu wangependa kuzungumzia suala hili lakini ni vizuri tujue jinsi tutashirikiana kuimarisha shule za chekechea. Ni lazima pia tuwaboreshe walimu kwa kuwapa mishahara."
}