GET /api/v0.1/hansard/entries/698359/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 698359,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/698359/?format=api",
    "text_counter": 226,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Nassir",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2433,
        "legal_name": "Abdulswamad Sheriff Nassir",
        "slug": "abdulswamad-sheriff-nassir"
    },
    "content": "Ahsante sana, Naibu Spika wa Muda. Leo, nimekuwa kitinda-mimba katika wazungumzaji. Nimekuwa wa mwisho kabisa. Kwanza, ningependa kutoa kongole kwa Seneti kwa kuuleta Mswada huu katika Bunge. Kwa sababu nimeusoma huu Mswada, ningeomba Kamati ya Elimu katika Bunge hili ipewe nafasi ya kuangalia sheria ya elimu iliyoko ili tuweze kuizingatia kikamilifu, haswa Ibara ya 35, ambayo inasema ni lazima kila shule iweke orodha itakayoonyesha ni watoto wangapi wameweza kupata elimu katika shule hiyo, na kuonyesha tarehe ya kuzaliwa ya kila mtoto. Vile vile, shule zinatakiwa kuonyesha jinsi watoto wanavyoweza kusoma, iwapo kuna watoto ambao wamelipishwa pesa zozote, jinsi masomo ya watoto yanavyoendelea, na chanjo walizopewa watoto na kadhalika. Hili ni jambo muhimu sana kule ninakotoka. Kutakuwa na ushahidi kwamba mzazi ameweza kujihusisha na maswala ya mtoto wake. Tukiendelea mbele, Ibara ya 39 inasema kwamba iwapo kutakuwa na kulipa karo, jambo hilo litekelezwe kwa watoto ambao si Wakenya. Watoto Wakenya hawapaswi kuzuiliwa kupata elimu kwa sababu ya kushindwa kulipa karo ya shule. Tukiendelea mbele, Ibara ya 41 inadhibitisha waziwazi, lakini baada ya kusoma Ibara ya 41(2), inasema kwamba mtoto ataweza kuingia katika shule ya chekechea kuanzia miaka mitatu mpaka sita. Lakini nimesoma katika Ibara ya 41(2) kwamba wamepeana ruhusa mwalimu mkuu anaweza kukubalia mtoto ikiwa amepitisha umri wa miaka sita. Hususan kule tunakotoka, kuna watoto wa umri mchanga wanaoanzishwa shule ya madrassa kisha wanaenda katika shule hizo. Ibara ya 46 inazungumzia yale masomo yatakayofunzwa katika shule za chekechea. Sasa hivi, kila mmoja anamsomesha moto wake anavyotaka, lakini Mswada huu unatupa mwelekeo. Ibara ya 51 inazungumzia kuhusu watoto wa shule za chekechea. Serikali za kaunti zitahakikisha kwamba watoto walioko katika shule za chekechea watapatiwa lishe bora ili watoto wetu wanawiri. Nikimalizia, Ibara ya 69 inazungumzia kuhusu watoto wetu wachanga. Kutandika watoto wachanga si vizuri. Sheria hii inaweka wazi ikiwa utaamua kuchukua sheria mikononi mwako na utandike ama umtese mtoto akawa na bughudha ndani ya kichwa chake, basi utafungwa kifungo kisichozidi miaka minne. Ama utalipa dhamana isiopungua Kshs500,000, ama vile jaji atakavyokuhukumu pia unaweza kuhukumiwa yote hayo mawili kwa pamoja. Huu ni Mswada mzuri. Ningeomba Kamati yetu ya Elimu iaangalie vipengele kama hivi viingizwe katika sheria yetu ya elimu. Kwa hayo machache, nasema ahsante sana."
}