GET /api/v0.1/hansard/entries/698792/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 698792,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/698792/?format=api",
    "text_counter": 91,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante Bw. Spika. Sheria katika nchi hii iko wazi; ikiwa mfanyikazi wa Serikali ambaye anatakikana kumiliki chombo ambacho kinaweza kuhatarisha maisha, kunao umuhimu achukue majukumu wakati maisha ya mtu yamehatarishwa. Kulingana na majibu aliyosoma Mwenyekiti, ni kwamba hawana pesa za kugharamia maumivu ambayo huyu msichana aliweza kuathirika na ile risasi. Swali ni; katika mahakama zetu za Kenya, kila mtu anayepatikana na hatia ya kwamba aliweza kutupa risasi na ikaathiri Mkenya mwingine, serikali iko na jukumu la kuchukua wadhifa huo na kuona ya kwamba mtu huyo amefidiwa Imekuwaje Mwenyekiti hivi sasa anakuja na majibu ambayo ni aibu katika wizara iliyoko katika wizara ya Serikali ya Ofisi ya Rais kwamba leo askari anaweza kupiga risasi mtoto wa kike? Askari anaweza kutoa mtu jicho halafu aseme hatuna pesa ya kulipa? Haya ni madharau ya aina gani? Kwa hivyo, sisi kama Seneti, tunakuomba, Bw. Spika, uchukue wadhfa huu wa kuweza kuweka msimamo kikamilifu wa Seneti. Ikiwa hatua kama hiyo ichukuliwe, askari huyo awachishwe kazi na apelekwe mahakamani na achukuliwe hatua na Serikali iweze kumfidia yule aliyeathirika. Asante sana."
}