GET /api/v0.1/hansard/entries/699131/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 699131,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/699131/?format=api",
"text_counter": 64,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Onyonka",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 128,
"legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
"slug": "richard-onyonka"
},
"content": "Asante Mhe. Spika. Ninakumbuka tulilizungumzia jambo hili la mishahara ya Wabunge ambao walikuwa katika Bunge hili hapo awali mwaka wa 2012. Wakati ule, tuligundua Wakenya wanadhani Wabunge wanapewa hela nyingi zaidi na haziambatani na hela ambazo wananchi wengine wanapata. Ningependa kusihi Bunge hili kuwa vile wenzangu wamezungumza, na ukiangalia mwaka ujao, utaona kwamba asilimia 80 ya Wabunge ambao wako hapa hawatarudi. Huo ndio muongozo ambao tunaona kila mwaka. Asilimia 80 au 75 ya wale Wabunge wanachaguliwa hawarudi hapa. Jambo muhimu ni kuwa ukiwaangalia wazee na akina mama ambao walikuwa Wabunge katika hili Bunge, utaona kwamba wana shida sana. Hawapati matibabu hospitalini na hawana hela ya kununua mafuta ya magari yao. Hata hawana magari kwa sababu wengi wao walikuwa wakifanya siasa wakati Hazina ya Ustawi wa Maeneo Bunge (CDF) haikuwepo. Ningependa kusihi Bunge hili lihakikishe limerekebisha hii shida ambayo imekuwa ikiwakera Wabunge wa zamani. Vile ndugu yangu, Mhe. (Dkt.) Nyikal amesema, ni vyema tuhakikishe kuna usawa wa mishahara ya Wabunge wa wakati huu na wafanyakazi wote wa Serikali. Hili likitendeka, kila mtu atakubali kuwa anapata riziki ile ambayo sheria inamkubalia kupata. Kumalizia, ningependa kuwaambia wale Wabunge ambao wako hapa sasa kwamba ingawa hili jambo linawakera wale wazee na akina mama ambao wamekuwa hapa awali kuliko sisi, wembe ni ule ule utatunyoa. Asante sana ndugu Spika."
}