GET /api/v0.1/hansard/entries/699392/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 699392,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/699392/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika, ninataka kumshukuru Mhe. Haji kwa taarifa aliyoileta hapa Bungeni kuhusu jamii ya Makonde. Kupitia uongozi wa Spika wa Bunge hili jamii hii itapewa vitambulisho. Walipata masaibu mengi sana jana walipotoka Kwale kuja hapa Nairobi kuwasilisha malalamiko yao katika ofisi ya Rais. Wakiwa njiani walipata shida nyingi . Walishikwa pale Voi na Kwale. Walinyaganywa funguo za magari yao na hata pesa walizokuwa nazo mifukoni. Bw. Spika, hawa ni wananchi wanateseka. Nikiendelea kuzungumzia mambo yale yamesemwa na Sen. Haji, ninaomba Wasomali wote pahali walipo wabadilishe jina lao. Ni afadhali wajulikane kama Waria. Kwa mfano, mimi nikienda Tanzania na ninataka kuishi huko nitabandikwa jina la Mkenya, lakini nitapewa kitambulisho cha Tanzania. Kwa hivyo, Wasomali wanaoishi hapa kutoka nchi ya Somalia wajiite Waria wa Kenya ili wapate vitambulisho na huduma zingine. Ukisema Msomali ni Msomali na wakutoka Somalia, basi hiyo italeta utata."
}