GET /api/v0.1/hansard/entries/699397/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 699397,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/699397/?format=api",
"text_counter": 134,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Bw. Spika, kwanza naomba kumpongeza kakangu, Sen. Haji. Ukweli ni kwamba mnyonge anyongwe lakini haki yake apewe. Mimi ni mzaliwa waVipingo. Jamii ya Makonde wanaishi Vipingo. Kwa hiyo, nitavaa junga niungane na jamii ya Makonde kwa sababu mimi nililelewa nao kule Vipingo. Makonde walikuwa wakikata makonge kule Vipingo. Tumekaa na wao Vipingo miaka mingi sana. Wazazi wao na babu zangu walikuwa wanafanya kazi mahali pamoja, Kwa hivyo, ni huzuni kubwa kuona mimi nimekuwa Seneta na niko hapa na watu wangu ambao tulicheza nao nikiwa mchanga hawana vitambulisho. Ningekuwa nimetoka nje, watu wangeshangaa labda imekuwaaje kwa sababu ni watu ambao tulilelewa pamoja. Kwa hivyo, lazima tuona vile ambavyo tutawachukua kama jamii yetu. Ni watu wa kufanya kazi kwa bidii sana. Jamii yetu si wafanya kazi kama watu wa jamii ya Makonde. Kwa hivyo, hawa ni ndungu zetu, watoto na wazazi wetu."
}