GET /api/v0.1/hansard/entries/699531/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 699531,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/699531/?format=api",
"text_counter": 268,
"type": "speech",
"speaker_name": "Sen. Kisasa",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13124,
"legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
"slug": "mshenga-mvita-kisasa"
},
"content": "Bw. Spika wa muda, ninampa pongezi Sen. Kagwe. Unamwona ana simanzi nyingi anapotukumbusha kuhusu teknolojia. Naomba kutoa hongera kwa Serikali yetu. Kama unavyojua, akopaye deni akilipa huwa ameondoa lawama. Kwa hivyo, vile Serikali ilivyokuwa imeahidi kuwa itapaeana vipakatalishi kwa watoto wetu, hilo ni deni ambalo linaendelea kufutwa. Kama mama, ama mzazi na wale mama wengine, sote tuna raha kubwa kwa sababu watoto wetu wameondolewa ule mzigo wa vitabu waliyokuwa wanabeba hadi mwendo ukabadilika. Pia, walijipata wafupi kwa mzigo mkubwa wa vitabu, lakini teknolojia itapunguza ile bughdha ya kubeba mzigo mkubwa sana wanapoenda shule ama kurudi nyumbani. Bw. Spika wa Muda, teknolojia ni wapi haitumiwi; iwe ni sokoni, hospitalini ama shuleni. Siku hizi ni rahisi sana kuwasiliana. Kila mzazi anawezakupewa habari ya mtoto wake anavyoendelea ama akapewa ripoti ya karo ilipofikia bila kujaza mafaili tele ofisini mwetu. Hata kwenye hospitali, mambo yamekuwa rahisi hivi kwamba, si lazima uende hospitalini ndio upate tiba. Tuseme umeenda Agha Khan Kisumu, siyo lazima uende mpaka Agha Khan, Mombasa. Unaweza kutibiwa popote pale kwa sababu ya teknolojia kwa kubonyeza kidude na kila jambo kuhusiana na yule mgonjwa litaletwa pale karibu naye. Teknolojia imeturahisishia kazi. Ninaomba kutoa shukrani sana. Kongole kwa Serikali yetu kwa kutoa ile mitambo ya Kisasa. Je, tuna ujuzi na teknolojia hizi ambazo zimeletwa? Kwa hivyo, tuone ya kwamba kila kaunti lazima ivae njuga na ijue kuwa hakuna mawimbi yanayongojea mtu yeyote. Lazima mawimbi yatatubeba. Kila kaunti lazima iwe na eneo ambalo limetengewa kiteknolojia ili iwe rahisi kwa wagonjwa wetu. Nimeongea kuhusu shule na supermarkets ambako huna budi kubeba pesa taslimu kwa sababu unaweza kuvamiwa na magaidi ama walinzi wako. Ukifika ni kutoa kadi na kulipa bili yako. The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}