GET /api/v0.1/hansard/entries/699533/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 699533,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/699533/?format=api",
"text_counter": 270,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Pia, tuangalie upande wa vilipuzi ama usalama.Vile vilipuzi vinatumiwa kiteknolojia. Vijana wetu wanatakiwa waende kwa mafunzo kama hayo ili tusitishwe na Al Shaabab ambao wanatumia vilipuzi kwa kutumia teknolojia ambayo sisi wenyewe hatujui kuvizuia vile vilipuzi. Kwa hivyo, tunaona ya kwamba lazima tuwe wajuzi wa teknolojia ili tuone ni nini tutalofanya ikiwa tumekabiliwa na shida kama hizo. Lazima bajeti iweko kwa sababu mkono mtupu haulambwi. Lazima kila kaunti na Serikali kuu zitenge maeneo fulani kwa mafunzo kama hayo. Kila kaunti iwe itaweka pesa kwa sababu chanda chema lazima kivikwe pete. Tuone ya kwamba kila kaunti itaweka pesa ambazo zitatosha kwa sababu pesa adimu hazitatusaidia. Ni lazima tuichukue teknolojia kama kitu ambacho tutakiweka mbele. Mbwa hawezi kukuuma ukimjua jina. Kwa hivyo, laazima tuikubali teknolojia kama kitu kizuri kwetu. Bw. Spika wa muda, kuna watu wengi wanaoiogopa teknolojia. Hadi leo kuna watu ambao hawataki simu. Mtu anataka kitu ambacho atakishika mkononi lakini akiambiwa: “Huu ujumbe utakufuata.” hataki. Lazima sisi kama Wakenya tukubali kwenda na vile hali ilivyo kwa mageuzi, sambamba na nchi zingine. Tusikubali kuwekwa nyuma. Wakati ni ukuta, na mtu akipigana nao ataumia mwenyewe. Nimeinuka hapa ili kusema kwamba, lazima tuichukue teknolojia kama kitu ambacho sasa hivi kila mtu amebadilika. Lazima sote tubadilike na kutafuta njia ambayo ni nyepesi kwetu ili tuishi katika nchi yetu. Sisi huwa na aibu sana tukienda nchi za nje tukiona wenzetu walivyo mbele. Ukiangalia mabasi yenyewe hujirudisha chini ili wenye baiskeli wapande kwa urahisi. Huna haja ya kupiga kengele kusema basi isimame kwa kuwa maandishi yajipitisha yenyewe. Twalia kwa sababu tuko nyuma kiteknolojia. Bw. Spika umesikia Sen. Kagwe akilia na kushangaa. Anaona aibu mbona sisi bado tuko nyuma. Hii ni kwa sababu hapa kwetu tuko nyuma kwa sababu hatutaki mawazo mapya. Kama unavyojua, kipya kinyemi. Kwa nini tusifuate kitu kipya? Kwa nini tusigange yanayokuja kwa sababu yaliyopita si ndwele? Nawaambia wenzangu na watu wote kwenye kaunti kwamba tuwe tukiletewa vitu vipya tuvikubali ili teknolojia itupeleke mbele. Pia mawasiliano ni teknolojia. Yanatufuata mpaka nyumbani mwetu ama vyumbani mwetu. Hata hivyo, hii teknolojia yatupeleka mrengo mwingine kwa sababu utaona inachukua wakati wetu mwingi sana na kuachana na familia zetu. Vile tunavyotaka teknolojia, lazima tuivalie njuga. Tuangalie kuwa ni lazima tujumuike na familia zetu na tusiwe kwenye mtandao sana. Pia, tuletewe teknolojia ambazo hazitakuwa mbaya kwa miili yetu. Bw. Spika, mengi siku hizi huenda rahisi sana kwenye mtandao. Kwa mfano, hakuna ugonjwa ambao huwezi kuuangalia kwenye Youtube. Jana nimeeshangaa nilipokuwa naangalia tiba ya ugonjwa fulani. Mara hiyo, nikaona kwamba teknolojia imenisaidia. Nilienda jikoni kwangu saa hiyo hiyo na nikaelekezwa kwamba niongeze tumeric yaani bizari mbichi, halafu niongeze chumvi ambayo iko kwenye kila jiko la mwanamke. Kwa hivyo, hii teknolojia imetuletea mambo mazuri. Imetutoa kwenye ujinga. Wakati mwingine huwezi kuenda mahali fulani kwa sababu mawasiliano yatakufuata mpaka pale pale nyumbani. Itakufanya usitumie pesa kusema lazima uende mji fulani au nchi fulani. Ukifika kule utakuwa umeangalia na kujua daktari amesema nini. Zamani, daktari angekuja, aongee - wajua madaktari wanaongea ni kama wale wengine The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}