GET /api/v0.1/hansard/entries/699535/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 699535,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/699535/?format=api",
    "text_counter": 272,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "hawajaenda shule - Kiingereza lakini hujui anachosema. Siku hizi, teknolojia imetufanya kwamba daktari akisema jambo unaweza kuangalia wakati huo huona ujue huo ugonjwa ulivyo, vile utakavyotibiwa na athari zake ni gani. Ninamuunga mkono Sen.Kagwe na ninaomba tuende mbio na sisi, tucheze kwa mtindo mmoja na nchi zingine kwa kuwa teknolojia ikituacha, tutakuwa tumeachwa nyuma.Teknolojia ni mawimbi ambayo hayatatungojea kamwe. Kwa hivyo, lazima na sisi tuwe palepale kwenye ufuo wa bahari ili tusaidike. Ni lazima vijana wetu walio kwenye jeshi watoke nje na kusoma kuhusu vilipuzi. Uliona tulichelewa siku za Westgate kwa sababu vijana wetu hawakuwa na ile teknolojia. Uliona tulichelewa kwa sababu vijana wetu hawakuwa kwenye teknolojia. Ilibidi watu watoke nje. Unaona ni gharama iliyoje kuchukua watu ambao wako nje wanaojifanya wana ujuzi na sisi tunaujuzi. Pia, kama nilivyosema vipakatalishi zimekuja wakati mzuri. Ukiangalia mpaka pale nyuma, watoto wetu akili zao ni chapchap kwa sababu ukishindwa na kitu kwenye simu, itabidi uite kijana. Kama unavyoona, Serikali imezingatia mambo ya vijana wetu kwa kuona kuwa lazima wapewe vipakatalishi, lazima wawe na ile elimu ambayo mtoto mwingine yeyote ama lazima apewe ule wakati mwafaka kwa sababu ukipata kipakatalishi kutokea darasa la kwanza, watoto wetu hawatakuwa bure bali watakuwa wataalamu. Kwa hivyo, Bw. Spika wa Muda, mimi kama mama ninasema hongera sana. Hii teknolojia isambazwe hadi kila shirika liweze kuwa na teknolojia ambayo inahusiana na ile kazi mtu anafanya. Kwa hayo mengi, ninasema shukrani na nampa pongezi Sen. Kagwe."
}