GET /api/v0.1/hansard/entries/699895/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 699895,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/699895/?format=api",
    "text_counter": 143,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 98,
        "legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
        "slug": "thomas-mwadeghu"
    },
    "content": "Ahsante Mhe. Spika. Naomba kuunga mkono Hoja hii ya mabadaliko ya Wabunge katika nyadhifa mbalimbali za kamati. Kama unavyoelewa, imebidi mara nyingine tuje mbele ya Bunge tuombe kibali cha kupatia Wabunge kamati mbalimbali kulingana na uzito wa kazi vile ulivyo. Kama tunavyoona, tuko na Mhe. Opiyo Wandayi, ambaye kama mnavyojua kuna wakati alikuwa na tatizo. Kwa hivyo, tunamrudisha maana tulikuwa tumekwishapeana nafasi katika kamati mbalimbali. Imebidi basi tufanye mabadiliko na ukarabati ili angalau nafasi zipatikane ndiposa kila moja apate nafasi yake. Tumejadiliana na ikatubidi tufanye mageuzo yanayowahusu wenzetu katika kamati mbalimbali ili wapate kupelekwa kufanya kazi katika kamati nyingine. Wapo wengine walioomba ruhusa wabadilishiwe kamati kwa sababu labda kazi zimewazidi ama wangependa wapate kuelewa zaidi kazi katika kamati nyingine. Kwa hivyo, imebidi tufanye mageuzo haya na ni ombi langu kwenu Wabunge wenzangu mwapatie kibali ili wapate nafasi ya kuhudumu katika kamati hizi. Iwapo itabidi, tutarudi hapa Bungeni tena kuleta mageuzo mengine ili kila Mbunge apate nafasi ya kuchangia kikamilifu katika shughuli za Bunge. Naunga mkono."
}