GET /api/v0.1/hansard/entries/700368/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 700368,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/700368/?format=api",
    "text_counter": 69,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Mwanyoha",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 2308,
        "legal_name": "Hassan Mohamed Mwanyoha",
        "slug": "hassan-mohamed-mwanyoha"
    },
    "content": "Ni haki hii stakabadhi itolewe bure kwa sababu tayari mtu amefanyiwa madhara au dhambi. Si vizuri tena atafute pesa anunue stakabadhi hii. Ninawaomba Wabunge walio hapa waipitishe Hoja hii. Jambo hili linafaa lifuatiliwe sawasawa kwa sababu mbali na kuwa unatakikana ulipe ile ada ambayo ni ya Serikali, bila kitu kidogo polisi hawakupatii P3 Form. Kwa hivyo, ni bora wale wanaohusika wahakikishe kwamba shahada hii inatolewa bure, na iwe bure kweli. Si bure na Serikali ikose kile ilichokuwa ikipata lakini mtu binafsi anapatiwa kitu kidogo ndio atoe P3 Form. Hiki ni kitu ambacho kila mwananchi ana haki ya kupata ili haki iweze kuzingatiwa. Mhe. Naibu Spika wa Muda, ninaunga mkono Hoja hii ambayo imeletwa na Mhe. Omar Mwinyi, na ningependa itekelezwe mara moja. Asante."
}