GET /api/v0.1/hansard/entries/700449/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 700449,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/700449/?format=api",
    "text_counter": 150,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. Onyonka",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 128,
        "legal_name": "Richard Momoima Onyonka",
        "slug": "richard-onyonka"
    },
    "content": "Naibu Spika wa Muda, kwanza, ningependa kutoa ahsante zangu kwa Mhe. Richard Makenga ambaye alikuwa mbele yangu katika orodha, lakini amenikubalia nizungumze kwa sababu nina mahali ambapo nahitajika baada ya dakika 15. Pia, ningependa kutoa asante zangu kwa Mbunge mwenzangu Mhe. Omar Mwinyi kwa sababu Hoja hii ni ya heshima sana. Mambo tunayoyazungumzia ni yale ambayo hayawahusu wananchi ambao hawajiwezi. Ni mambo ambayo saa zingine tunayaangalia na kusema hakuna haja ya kuyashughulikia; tuyaangalie yale mengine makubwa. Jambo la kuwa na hati mtu akiumia ama akipigwa ni muhimu. Lazima mtu aende hospitali achukue ile hati ambayo itatumika kortini kama kuna kesi. Hati hii lazima iandikwe na daktari na itaonyesha vile mtu ameumia. Hili ni jambo muhimu na ni jambo ambalo tumeliachilia kama Wabunge na lilifaa kuangaziwa hapo mbeleni. Hiyo ndiyo sababu ambayo imenifanya nikaseme kuwa ndugu yangu Mhe. Omar Mwinyi amefanya vizuri kuleta Hoja hii, ili tuizungumzie na tueleze Wakenya ili waelewe kwamba kuna mambo fulani ambayo imefika wakati lazima tujihusishe nayo na kujaribu kuyarekebisha ama kutoa suluhu. Ni mambo nyeti ambayo yanawasumbua wananchi wa kawaida. Kama vile ndugu zangu wamesema hapa, mtu akifariki, kupata ile hati ambayo daktari ameandika ili kuwe na upasuaji wa kuonyesha ni nini kilichosababisha mtu huyo kufariki ni ngumu sana. Hati hiyo inaonyesha sababu ambazo zilimuua mtu huyo. Yaweza kuwa aliumia, ama alikua mgonjwa ama kwa sababu nyingine. Kazi yetu sisi Wabunge imekuwa ni kuzika watu. Ni shida sana kwa familia masikini kupata Kshs6,000 za kulipa daktari ili afanye upasuaje. Upasuaji huu lazima ufanyike kwa sababu hati ya upasuaji huhitajika kabla ya kumzika mtu. Mambo hayo mawili yana uhusiano. Wabunge wenzangu wamesema ukitaka hati ya matibabu kwa hospitali, haiuzwi. Ningependa kuwaelezea wenzangu wajue kuwa wakati huu ukienda kwa hospitali, utaambiwa kuwa hati hiyo haiuzwi. Ukiwa Mbunge, hauwezi kuulizwa pesa hizo. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}