GET /api/v0.1/hansard/entries/700839/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 700839,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/700839/?format=api",
"text_counter": 351,
"type": "other",
"speaker_name": "",
"speaker_title": "",
"speaker": null,
"content": "Serikali au Auditor-General kama anavyojulikana katika lugha ya Kiingereza. Ripoti hizi ni za mwaka wa 2014/2015 kuhusu matumizi ya pesa za Serikali. Pia tutakuwa na nafasi ya kuzingatia ripoti zamu ya pili ya 2014/2015. Hiyo ni sababu moja ya kuunga mkono Hoja hii. Bw. Spika Wa Muda, ni lazima uelewe siasa imepotoshwa sana na wenzetu. Siasa imepotoshwa kwa hali ya kwamba wale ambao wako katika makaunti wamepotosha wenzao na kuwaaambia kwamba Maseneta wako Nairobi. Leo karibu Maseneta wote unapata wamelimbikiziwa lawama kwamba wako Nairobi kila wakati na hawana wakati wa kutengamana na watu wao mashinani. Lakini nawaambia watu wetu kuwa Bunge la Seneti liko Nairobi, haliko Kisii, Bungoma, Kwale, Nandi au Kirinyiga. Bunge hili linafanya kazi kutoka Jumatatu hadi Ijumaa. Sisi hutumia wakati mwingi katika Kamati zetu. Tunawaka wa kuja hapa Bungeni na kujadili mambo mengi. Kuna baadhi ya watu ambao hawafuati sera za Serikali katika kuwahudumia wananchi. Mfano mzuri ni matumizi ya pesa za CDF. Pesa hizi zipelekwa mashinani ili zisimamiwe na magavana na ule utawala wa kaunti uweze kuangazia matumizi yake. Maanake ni lazima uchague kama utakuwa upande wa utawala au uwe Mbunge. Hauwezi kuchanganya yote mawili. Sera hii ilianzishwa katika hizo karne zilizopita katika utawala. Unaulizwa, “Wewe kama Mbunge umefanya nini katika kaunti yako?” “Wewe Mbunge ulileta maendeleo yapi?” Mbunge anafaa awe hapa atetee kaunti yake na atetee eneo lake la Bunge ili Serikali ya Kitaifa iletee maendeleo fulani. Si kwenda kule kufanya harambee na kuwadanganya watu kila leo ni harambee. Kama ingekuwa harambee zinatatua shida za Kenya, basi Wakenya hawangekuwa na shida yoyote. Tumekuwa na harambee tangu 1963 mpaka leo. Tunafanya harambee na miaka nenda miaka rudi. Inafaa tubadilishe sera zetu za kiserikali tuweze kuweka maadili na tuweze kuweka haki na usawa Serikalini. Unaenda kufanyia watu harambee na wewe ni mkuu katika Serikali ya Kitaifa na katika kaunti. Badala ya kuboresha huduma za afya, unafanyia watu harambee ya kwenda kufanyiwa matibabu katika mataifa ya kigeni. Badala ya kuboresha skuli na vyuo vikuu vyetu wewe unafanyia mtu harambee ili aende akasomee nje ya nchi. Hizi ni sera na mienendo ya kiabunuasi. Wewe kama umepatiwa fursa ya kutawala wenzako pitisha sera ambazo utahakikisha kila mtu amepata huduma za afya za kisawasawa. Kila mtu amepata fursa ya kisawasawa katika maswala ya elimu. Hakikisha umeleta maji na hakikisha umeleta maswala ya makao. Kwa hivyo, tumeichafua siasa ya Kenya. Bw. Spika, lazima sasa kuitakasa na tubadilishe mtazamo na fikira za siasa za Kenya. Kama wewe ni Mbunge, watu waelezwe shughuli zako ni zipi na sisi waeleze zetu ni zipi katika Bunge hili. Kuna wengine hapa hata wazungumzi na wengine hata hawaonekani. Kazi yao ni kuzuru ofisi hii na ile ili wapate kandarasi na wawe na pesa za kutoa katika Harambee. Hiyo ni maendeleo. Juzi ripoti fulani ilisema tuna ukilishi wa Useneta na Mwakilishi wa Wanawake. Mwananchi anamuomba gavana, anakuomba wewe, anamuomba Mwakilishi wa Wanawake, anamuomba Mwakilishi wa wadi. Wakenya kama mnataka kujikomboa hamwezi mkajifanya miaka yote hamfahamu. Hawa wakenya wetu pia hujifanya hawafahamu kila siku. Tuwafahamisheni na tujifanye tunafahamu. Kila tukijifanya hatafahamu ndio wafisadi watatumiliki zaidi. Kila siku The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}