GET /api/v0.1/hansard/entries/700841/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 700841,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/700841/?format=api",
    "text_counter": 353,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "tukisema kwamba hatujui Seneta amechaguliwa kufanya nini na Mwakilishi wa Wanawake amechaguliwa kufanya nini, ndio kila siku tunaendelea kupiga sera za ufisadi. Bw. Spika, wewe unasema wewe ni kampeina wa miaka 20 wa mtu fulani na wewe mwenyewe hujafika popote. Unasema, “Nimejitoa umri wangu wote, afya yangu yote, nampigania mtu fulani kura yangu.” Miaka ishirini wewe badala ya kufuata serikali unatafuta mapeni vidogo vidogo. Ndio kwa sababu hujafika. Sasa ndio tukienda chini tuweze kuwaelimisha tusiwe kila wakati tunataka pia sisi kuwa na uzoefu wa siasa za duni. Mpaka siku ile mtu atachukua msimamo uanze kusema kwamba sera ya kiserikali na ya kitaifa lazima iendeshwe tofauti. Lakini sisi wengine pia tunajiweka hizi pressure. Wewe Seneta pia unajaribu kuweka vikao, unajaribu kuweka maharambee, unajaribu kufanya kila kitu ili pia wewe uonekane pia unajumuika na huku unajilemea zaidi, ufadhali sio wake. Leo Seneta akitaka kufanya kikao atalipia maji, atalipia venue, atalipia chandarua, atalipia kipasa sauti, atalipia kila kitu. Gavana akitaka kufanya kikao kile kile halipi hata ndururu yake kwa sababu jukua ni la serikali, kipasa sauti ni ya serikali, mobilization ni ya serikali, maji ni ya serikali, inspectorate ni ya serikali na kila kitu chote ni cha serikali. Usijitakilifishe, wafahamishe watu. Watu wetu lazima watoe masikio taka waanze kufahamu. Ni lazima watoe uchafu kwenye masikio ili waweze kufahamu. Miaka 50 baada ya kupata Uhuru, hatuwezi kujifanya kuwa bado hatufahamu. Lazima tuwe na mkazo na shinikizo. Tunapozidi kujifanya ya kwamba hatufahamu, watu wengine watatuibia. Hii ndio maana tunaendelea kuwachagua viongozi wafisadi. Kwa mfano, Sen. M. Kajwang ana masomo na maadili yake ni mazuri. Pia mtazamo na mchango wake ni mzuri lakini wananchi watatafuta mtu mwenye pesa kwa sababu Sen. M. Kajwang hajawafanyia chochote. Wananchi wanafaa kuangalia majukumu yake katika Katiba ya Taifa la Kenya. Anafaa kupimo na mizani yao kwa yale wanayoyafanya katika Katiba. Haya maneno yamenitia ukali leo kwa sababu niliona kongamano fulani katika kaunti moja jirani wiki iliyopita ambapo watu wamechezeana dosari. Ndugu zangu wapwani hawawezi kujifanya kwamba kila siku hawafahamu ilhali watu wote Kenya mzima wanafahamu. Wengine wanaishi katika umaskini lakini siku ya kura wanawapigia watu wao kura. Wapwani pekee yao ndio wanaojifanya kuwa hawafahamu hayo. Bw. Spika wa Muda, ni lazima tuambiane ukweli katika taifa hili. Tuko na sauti na fursa ya kwenda mashinani ili tuwahamasishe, tuwaelimishe na tuwaambie watu wetu ukweli. Miaka 50 baada ya Uhuru wenzetu wameamka na kufika Mtito Andei lakini wewe bado hujaamka. Kila siku tunasema kwamba tunaonewa na kuthulumiwa. Je, hakuna maskini katika maeneo mengine kama Nyanza, Mkoa wa Kati, Magharibi na Kaskazini Mashariki? Mbona wao wanawapigia kura wanasiasa wao ilhali hawajawafanyia lolote? Tunathulumu Waakilishi wa Wadi bure kwa sababu wameshindwa kutulipia karo. Wao ni waakilishi wa wadi na mnajua utajiri na umaskini wao. Wanaenda mbio kwa ajili yenu. Tulikuwa na Rais kutoka kabila la Kalenjin kwa miaka 24. Je, wakalenjin wote walipata nini kwa jumla? Mbona wao bado wanapiga kura kwa wingi? Waliamka kitambo. Ndugu zetu kutoka Mkoa wa Kati hujitokeza asubuhi kwa wingi kupiga kura. Mbona sisi hujifanya kwamba hatufahamu? The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}