GET /api/v0.1/hansard/entries/700843/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 700843,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/700843/?format=api",
    "text_counter": 355,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "Maseneta wanaotaka usaidizi wanafaa kutuita ili tuweze kuwafahamisha watu. Hali hii haifai kuendelea. Ndio maana wafisadi wanahongana na kila siku raslimali yetu inaporwa na sera zetu za kisiasa zinaendelea kudhalilika na kudorora. Bw. Spika wa Muda, tunafaa kutumia fursa hizi kuelimisha watu. Niite katika Kauti ya Nandi, Kaunti ya Nyandarua au Kaunti ya Homa Bay ili tuwaeleze na kuwasaidia watu kwa sababu Kenya imefika mahali pabaya. Masikini ni wengi na fursa yao kimaisha ni haba. Mtu anapozaliwa masikini fursa yake iko katika hali duni. Masikini akifaulu maishani hiyo ni kazi ya Mungu na sio Serikali. Hakuna fursa yoyote inayotolewa na Serikali. Inakera na kuudhi tunapojifanya kwamba sisi hatufahamu kwamba tunafaa kupiga kura kwa wingi kama wenzetu wanaojitokeza kwa wingi. Nilipokuwa namfanyia kampeni Sen. Wetangula kulipokuwa na uchaguzi mdogo, niliwauliza watu kwa nini wangempigia kura. Walijibu kuwa ni kwa sababu walikuwa na imani kwamba siku moja atakuwa Rais wa Taifa la Kenya na kuleta matumaini kwao. Sen. Kisasa, sisi bado hatujaamka. Tunalalamika na kujiuliza ni nini tumepata kwa miaka yote ambayo tumewafanyia watu kampeni. Kuwanfanyia watu kampeni sio biashara wala kazi. Ni lazima wanasiasa pia wabadilishe mtazamo. Watu wanafaa kujumuika ili kuendeleze maadili, mikakati na falsafa. Bw. Spika wa Muda, naunga mkono Hoja hii. Mungu akitujalia, tunafaa kushikamana kama Maseneta na twende katika mitaa na kaunti zetu kwa pamoja na tufahamishane ili watu waelewa jukumu la kila mtu katika Katiba. Mtu anapopata fursa, asijidhalilishe kwa kufanya kama wale wengine. Kila mtu afanye kwa kipimo na nguvu zake."
}