GET /api/v0.1/hansard/entries/700844/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 700844,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/700844/?format=api",
    "text_counter": 356,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Kisasa",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13124,
        "legal_name": "Mshenga Mvita Kisasa",
        "slug": "mshenga-mvita-kisasa"
    },
    "content": "Bw. Spika wa Muda, wimbi mkali hufuatwa na shwari kwa sababu wimbi huwa na nguvu zaidi. Tumekuwa mbioni kama Seneti. Sasa ni fursa yetu kurudi nyumbani. Mimi ninafuraha kwa sababu nitakuwa nyumbani. Nimefurahi zaidi kwa sababu ndugu yangu Sen. Hassan amesema kwamba atarudi nyumbani ili awaeleze watu ukweli. Kule kwetu kuna ugonjwa ambao unaitwa ‘ongea, danganya mpwani’. Ugonjwa huo unashika macho na mtu wa Pwani huwa haoni vizuri anaposhikwa na ugonjwa huu. Niwajibu wetu kama viongozi kurudi nyumbani ili tuwaelimishe watu. Ugonjwa huo unaposhika macho, hata Serikali itengeneze barabara, mtu wa Pwani hataiona ile barabara. Serikali imeleta maendeleo mengi Pwani, watu wa Pwani hawayaoni maendeleo hayo. Nimefurahi kwa kumsikia Sen. Hassan akisema kwamba kuna umasikini pia bara. Ugonjwa huu unapomshika mtu wa Pwani haoni hata vyeti vya mashamba. Maendeleo kama hayo hayako katika kaunti zote. Ugonjwa huu ulitokea kule Magharibi mwa nchi, lakini wenyewe wameanza kupona. Naomba turudi nyumbani ili tueleze watu wetu kuwa wenzetu wameanza kupona kutokana na ugonjwa huu. Mbona tunajitwika vitu ambavyo havituhusu? Maji matulivu huwa yana kina kirefu. Kwa hivyo ni lazima maji hayo matulivu yajulikane kuwa yana kina kirefu. Lazima tuwaelimishe watu wetu ili wachaguwe mrengo wa maendeleo. Nawapa kongole Rais wetu na Naibu wake kwa kutupa maendeleo. Nimetembea Bonde la Ufa na najivunia maendeleo mengi ambayo yamefanywa Pwani. Unaweza kudhani kamba Naibu wa Rais ametoka Pwani. Nilimtembelea dada yangu, Sen. Chelule, na nikahuzunishwa na hali ya barabara. Nikirudi nyumbani nitawaelimisha na kuwaeleza watu wangu kwamba sisi kama watu The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}