GET /api/v0.1/hansard/entries/700994/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 700994,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/700994/?format=api",
"text_counter": 129,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. Mwadeghu",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 98,
"legal_name": "Thomas Ludindi Mwadeghu",
"slug": "thomas-mwadeghu"
},
"content": "Asante, Mhe. Naibu Spika, kwa nafasi hii uliyonipatia ili nami nitoe mchango wangu kuhusu wakurugenzi wa CBK ambao wamehojiwa na Kamati yetu ya Fedha, Mipango na Biashara. Kwanza, napinga Ripoti hii. Nina sababu zangu kwa nini sikubaliani nayo. Sababu ya kwanza ni kwamba tunatafuta wakurugenzi wa CBK. Sina haja ya ukabila. Hata kama kuna ukabila ambao utaonekana, kama mheshimiwa aliyezungumza hivi sasa alivyosema, basi peaneni kwa watu wenye ufasaha wa kazi, ambao wanaelewa na wana kisomo cha kiuchumi. Lakini nikianza kuangalia hapa, naona labda ndugu yangu Ruparel ana kisomo, ujuzi, ufasaha na anaelewa kazi ya kiuchumi. Huyo sina shida naye kama mkurugenzi wa CBK. Hata huyu shangazi Nelius Wanjiru Kariuki, nikiangalia kisomo na ufasaha wake ni nafuu. Anao ujuzi. Angalau amesoma na ana uzoefu lakini hawa wengine wote siwaungi mkono. Ninashangaa mwenyekiti mwenzangu wa Kamati hii ambaye nimefanya kazi naye katika Bunge la Kumi na ni Mhasibu mwenzangu, ameleta majina haya hapa Bungeni. Sikubaliani naye. Nilifanya kazi CBK nilipomaliza chuo kikuu. Nishafanya kazi kwa miaka minne katika Benki Kuu kabla wengine wenu hawajazaliwa. Katika Mwaka wa 1976 nilikuwa mfanyakazi wa Benki Kuu na hamkuweko. Sasa mnataka niweke sahihi kuwa nimekubali hawa ambao mnatuletea hapa kama wakurugenzi wa Benki Kuu. Nitahukumiwa na hisia zangu nikikubali mambo haya ya kuletewa majina na kuambiwa kuwa huyu anatoka kwenu. Kama hana ujuzi au ufasaha ama kama haelewi kazi, sitaunga mkono. Hatutafuti wahasibu. Tungekuwa tunatafuta wahasibu, ningekubaliana na Ripoti hii. Hatutafuti wahasibu. Tunatafuta wakurugenzi ambao wataelewa jinsi uchumi unavyoendelea. Juzi, tumepitisha Mswada hapa wa kuhakikisha kuwa riba za benki zinapunguzwa ama zinasalia hapo zilipo. Ni sababu ya ufasaha wa ndugu yangu ambaye aliuleta Mswada huo hapa. Alikuwa anaelewa anazungumza kuhusu nini. Tukiangalia vile hali ya uchumi ilivyo na jinsi benki zinavyoanguka, hata mwanasheria ambaye ana uzoefu wa sheria za benki hayupo hapa na mnataka nikubali kuwa Kamati imefanya kazi nzuri. Naomba niikosoe bila kujali. Kwa maoni yangu, Kamati hii haikufanya kazi ambayo inatakiwa kufanywa. Kama CBK imekaa bila wakurugenzi kwa muda huu wote na hawa ndio wakurugenzi walioletwa ili waanze pale wenzao walipoanzia, samahani, naomba nitoe maoni yangu na ghadhabu ambayo imenishika. Nikiona ndugu yangu anaenda kuwania kiti cha ugavana na ananiletea majina haya, nasikitika sana. Hii Ripoti siiungi mkono na Kamati yenyewe pia naikosoa kwa kuleta kazi ambayo haifai kuletwa Bungeni na wametumia pesa za umma. Napinga Ripoti hii na wakurugenzi hawa. Kama ningekuwa na idhini, ningewaomba Wabunge wenzangu waniunge mkono kuwa hawa ambao wameteuliwa na Kamati hii hawana uzoefu na kazi hii na itawaletea shida. Baadaye ni sisi watu wa Kenya watakaolalamika kuwa CBK haifanyi kazi au haiendeshwi vizuri. Hivi sasa The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}