GET /api/v0.1/hansard/entries/701109/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 701109,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/701109/?format=api",
    "text_counter": 244,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13130,
        "legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
        "slug": "zuleikha-juma-hassan"
    },
    "content": "Shukrani sana Mheshimiwa Naibu Spika wa Muda kwa kunipatia nafasi hii kuchangia Hoja hii muhimu sana. Nataka kumshukuru Mheshimiwa Nooru kwa kuleta Hoja hii hapa Bungeni. Hili jambo limenitamausha sasa kwa kiasi cha wiki nzima. Nimehuzunika kusikia na kuona jinsi watu wanavyoteseka katika kaunti yangu ya Kwale. Hili jambo halijaanza jana, juzi wala wiki jana. Hii mvua ilipoanza miezi kadhaa iliyopita ilikuwa chache sana na kulikuwepo na dalili ya ukame. Kuna akina nyanya ambao hawajawahi kuenda shule lakini walitabiri kwamba mwaka huu kutakuwepo njaa. Itakuwaje wataalamu ambao wameandikwa kazi na Serikali hawawezi kujua kama huu mwaka kungekuwa na ukame? Hivyo, tungejitayarisha mapema kwa chakula na maji. Mimi nimezunguka sehemu za Kaunti ya Kwale. Katika wadi ya Puma nilipata wanawake wakanieleza kuwa kuna njaa. Wao huamka asubuhi lakini hawana chai, wala chakula. Wao hushinda hivyo mchana kutwa bila chakula. Ifikapo jioni, bado huwa hawajala chochote. Wana watoto wadogo. Ni ajabu kwamba mtoto wa miaka miwili au saba anaishi bila chakula! Saa hizi hamna chakula kwa sababu mvua haikutosha. Mahindi hayakupatikana. Maji hayapo na yakipatikana ni mwendo mrefu sana. Lakini watu wanaenda wakiteka maji ya chini ambayo ni machafu. Hivyo ndivyo wanasukuma gurudumu la maisha. Hivi sasa yale maji ya chini yamekauka kabisa kwa hivyo hawana njia yoyote ya kupata maji safi. Bila shaka kama hakuna mtu ama shirika lolote ambalo limeenda kujua kama kuna watu wamefariki kwa sababu ya hili janga, nina hakika watu wamefariki maanake wiki zilizopita nilienda nikaonana na watu wagonjwa wanaomeza dawa lakini hawana chakula. Bila shaka kuna watoto na wengineo ambao wameathirika . Pia nimepata habari kutoka kwa Wadi ya Kasemeni ya kuwa Serikali ya Kaunti imejenga sehemu za akina mama kujifungulia katika zahanati, lakini zahanati hazina maji. Hivi sasa nimeambiwa kuna wanawake wanajifungua watoto na hakuna hata maji ya kuosha mtoto. Vile mama alivyojifungua ndio vile anarudi aende mpaka nyumbani kwa sababu hakuna maji. Hivi sasa mifugo; ng’ombe, mbuzi na kadhalika wanafariki, kitu ambacho ni mali ya hawa watu wa Kwale ambao wanaishi sehemu za Kinango, Lunga Lunga na baadhi ya sehemu za Matuga. Hata mvua ikija watakuwa wamepata hasara sana. Ninashangaa, kama chama chetu cha ODM kimeweza kutetea ugatuzi ukaja tukafaulu na ukapita, kuna shida gani? Pesa zimetolewa na Bunge za Seneti na Taifa na Bunge hili letu wamehakikisha kuwa senti zinafika kaunti lakini miaka mine sasa kaunti hazijaweza kufanya miradi ya kudumu katika hii sehemu. Kuna sehemu zina maji lakini zingine zina ukame zaidi. Ingekuwa vyema hizo kushughulikiwa. Saa zingine wanalaumu kuwa maji ya sehemu ya chini yana chumvi lakini saa hii tunajua ya kuwa kuna tecnolojia za kuweza kutoa chumvi kwenye maji. Hivi sasa afadhali maji ya chumvi kuliko kukosa maji kabisa. Kitu kingine wanachosingizia, wanasema pesa nyingi inatumiwa kwa maji ya pipe ."
}