GET /api/v0.1/hansard/entries/701116/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 701116,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/701116/?format=api",
"text_counter": 251,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Juma",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 13130,
"legal_name": "Zuleikha Juma Hassan",
"slug": "zuleikha-juma-hassan"
},
"content": "Asante sana. Jambo lingine ni kwamba kaunti wamesema watachimba yale madimbwi ya maji lakini mpaka sasa kuna madimbwi mengi kama huko Kaunti ya Kwale ambayo hayajachimbwa. Unajua mchanga huo unarudi ndani na hawajakuja kuutoa katika miaka minne na wala hawajachimba lile dimbwi likawa linaweza kubeba maji mengi kusaidia watu. Jambo lingine, nataka kutumia hii nafasi kuwaeleza wananchi kuwa huu ndio wakati wa kujua kiongozi anayekujali, maanake hakuna kiongozi mzuri ambaye atakubali watu wake wafe, rasilmali zao zife ama ziharibike na watu waishi kwa dhiki kama hiyo ya kuwa hakuna chakula na hivi sasa pia hakuna maji ya kunywa. Nataka kuomba Serikali kuu na ile ya kaunti kama wamekuwa wamezembea kazini---"
}