GET /api/v0.1/hansard/entries/701127/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 701127,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/701127/?format=api",
    "text_counter": 262,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Yafaa ieleweke kwamba tulipopitisha Katiba na kupigia kura ugatuzi, ilikuwa kwa sababu wananchi wapate huduma za karibu. Inasikitisha kwamba huduma ya karibu ambayo wananchi wa majimbo mengi wameweza kupata ni kule kuona magari ya kifahari na makubwa makubwa ambayo mara mingi hupita na kuwachia vumbi wasijue wanakotoka ama wanapokwenda. Laikipia inajulikana kwa umaarufu wake wa kufuga mifugo wa hali ya juu, haswa ng’ombe wa nyama. Pia, tumejulikana kwa kuhifadhi nyasi na maneno yetu mengine. Imekuwa ni kitu cha kusikitisha kwamba sisi tumehifadhi nyasi zetu kupitia conservancies ili tupeleke mifugo wetu pale wakati wa njaa. Lakini, hali kule imekuwa ni mwenye nguvu mpishe. Kumekuwa na tatizo kubwa ambapo jirani wetu kutoka anakotoka mamangu hapa na wengine kutoka Isiolo ni kutumia nguvu kutupokonya zile rasilimali tumeweza kutunza."
}