GET /api/v0.1/hansard/entries/701150/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 701150,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/701150/?format=api",
    "text_counter": 285,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Leshoomo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 379,
        "legal_name": "Maison Leshoomo",
        "slug": "maison-leshoomo"
    },
    "content": "Katika Kaunti yangu ya Samburu tumepoteza watu kadhaa kwa sababu ya ndovu ambao wanang’ang’ania maji na tumeshindwa kutatua hilo jambo. Hii ni kwa sababu kaunti zimepewa pesa na ukiangalia sehemu zingine haziangalii shida za watu wao. Katika Samburu Kaunti, miaka nenda miaka rudi, shida ni njaa na maji. Saa hii watoto wamefunga shule mapema kwa sababu ya maji. Kama leo nimejitolea kuwachotea wafugaji maji, ningependa kuuliza: Shida iko wapi kwa sababu kaunti ziko na pesa? Pia tunaomba Serikali yetu kuu iweze kuangalia hizo pesa ambazo zinatumwa kwa kaunti zinatumika kwa njia gani."
}