GET /api/v0.1/hansard/entries/701455/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 701455,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/701455/?format=api",
    "text_counter": 297,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Uunajua vitinda mimba wako namna hiyo kila siku. Itakuwa vyema kama serikali za mashinani zitapewa pesa za kutosha ili zijenge maktaba ya kuifadhi vitabu vya watoto wetu ili waweze kusoma. Huduma hii ya vitabu wakati huu iko mikononi mwa Serikali ya Kitaifa. Huduma kama hii isimamiwe na serikali za mashinani maanake mtu anayevaa kiatu anajua pale kile kinamuuma zaidi. Bw. Spika, hata elimu ya msingi inaweza kusimamiwa na serikali za mashinani watoto wengi kule mashinani wapate elimu bora. Kwa hayo machache, ninaunga mkono Hoja hii kwamba huduma za barabara ziwe chini ya serikali za ugatuzi ama serikali za mashinani."
}