GET /api/v0.1/hansard/entries/701534/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 701534,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/701534/?format=api",
    "text_counter": 376,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Muthama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 96,
        "legal_name": "Johnson Nduya Muthama",
        "slug": "johnson-muthama"
    },
    "content": "Bw. Spika, nashukuru.Naunga mkono mjadala huu kwa hali na dhati. Maajabu hayaishi Kenya yetu. Nina shangaa nilini tutapata viongozi kama marehemu John Michuki. Katika Bunge la kumi, mradiwa maji wa Murang’a uliletwaBungeni. Katika taarifa ya uwazi, marehemu John Michuki alisema mradi huo utajengwa akiwa kaburini. Maneno yake yametimia kwa sababu aliaga na mradi unatimizwa. Jambo la kuhuzunisha na kushangaza ni kwamba, nilini viongozi wa taifa letu wata fikiria na kufanya mambo ambayo yana lenga masilahi na mahitaji ya wakenya pahalipo pote walipo. Bw. Spika, kiti unachoka kimeekaliwa tangu mwaka wa 1963. Kabla hujazaliwa, chanzo cha maji mahali unawakilisha ni pahali pale ulipowacha baada ya miaka 53. Hivi sasa, maji ya mto Athi yanatoka hapa mpaka baharini. Ni kilomita 18 kutoka Nairobi unapata maji ya mto Athi. Kutoka mto Sagana mpaka hapa, ni kilomita 78. Haya maji yote yanaelekea baharini na sisi tunaenda Murang’a kuchota yale maji machache na kuyalete hapa Nairobi. Watu wa Murang’a ambao ni majirani wangu hawana hata tone moja ya maji. Swali ni hili: Je, Serikali ya Jubilee inawafanyia kazi Wakenya walio na shida ya maji? Ni maendeleo gani imefanyia Wakenya kwa jumla? Mambo yao ya kuleta maendeleo ni kuumiza yule mnyonge ambaye anastahili kusaidiwa. Hii ni kishashe na sarakasi. Bw. Spika, jambo la kuhuzunisha ni kwa kwamba maji ya Murang’a inakusudiwa kutumia katika Jiji la Nairobi. Ni nani mpaka leo ameweza kuishi bila maji katika mji huu? Sisi tunaishi hapa na hatujasikia hata sauti ya mtu mmoja akisema hana maji. Leo tunashangaa Serikali ya Jubilee inakopa Kshs835 milioni kila mwezi kuendeleza miradi ambayo haimfaidi mwananchi wa Kenya hata kidogo. Reli ambayio inajengwa kutoka Pwani hadi Nairobi haisaidii mwananchi wa kawaida. Kwa mfano, ukisafirisha magari yako hadi Nairobi inamsaidia aje mwananchi wa Nandi na hana chakula, mahali pa kupeleka watoto wake shule na hata hospitali. Ni mradi tu. Huko tunasema Serikali ya Jubilee imefanya kazi ya kusaidia Wakenya. Hii ni miradi ambayo haifai wawachane nayo ikiwa wanataka kuwasaidia wananchi. Wakati The electronic version of the Senate Hansard Report is for information purposes only. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor, Senate"
}