GET /api/v0.1/hansard/entries/701536/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 701536,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/701536/?format=api",
    "text_counter": 378,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "kiongozi Raila Amolo Odinga anaposema miradi hii inaathiri mwananchi na inaumiza wananchi wa Kenya, sisi wengine tunataka kufanya siasa. Fikiria ya kwamba Waziri Wa Maji mhe. Eugene Wamalwa, anasema ya kwamba atatoa Kshs50 milioni kwa kila Mbunge ili wanyamaze. Haisemekani kwamba hiyo pesa inapeanwa katika sehemu ya uwakilishi wa Bunge, ni dhahiri na wazi inapewa Mbunge ili anyamaze. Ni ukweli wamenyamaza kwa maana hata wale watu wanatoka Mkoa wa Kati ambao wanapiga siasa chinichini wakizungumzia huu mradi, hakuna hata mmoja yuko hapa. Wote wametoka na kwenda ili kuonyesha ya kwamba wanaunga Serikali ya Jubilee mkono. Serikali na maendeleo ya wananchi ni tofauti. Mtu akisimama na kusema ya kwamba analinda Serikali yake anafaa aangalie hii Serikali inasaidia watu wake namna gani. Mnyonge Kenya yuko hatarini. Mnyonge Kenya hana sauti. Kwa mfano, watu wa Murang’a tumeona wakiongea kupitia vyombo vya habari. Mwananchi wa kawaidia anauliza itakuwa aje Serikali inachukua maji kutoka Murang’a na kupeleka Nairobi na sisi hatuna hata tone ya maji. Lakini hawepewi jibu kama hilo. Tunachosikia ni ya kwamba maji yanakuja Nairobi. Gavana wa Nairobi hana habari kamwe kama kuna maji yanayoletwa Nairobi kutoka Murang’a. Bw. Spika, naomba dakika mbili au tatu."
}