GET /api/v0.1/hansard/entries/702005/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 702005,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702005/?format=api",
"text_counter": 319,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Amolo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 631,
"legal_name": "Rachel Ameso Amolo",
"slug": "rachel-ameso-amolo"
},
"content": "ambaye tumekuwa tukisoma tukiwa katika shule za chekechea. Kweli ndugu zetu Wabunge wa kiume wangekuwa na nia ya kutusaidia ili idadi ya akina mama iongezeke katika Bunge letu la kitaifa, wangetupatia namna ya kufanya hiyo hesabu ili tuweze kujua moja ukiongeza moja utapata mbili. Lakini hapa hawajatuelezea lolote. Inamaanisha kwamba hili neno “pole pole” ama vile wameliweka katika lugha ya Kimombo ‘progressive’ ni njia moja ambayo hakuna lolote litatendeka hata kesho kutwa. Kwa hivyo, ingekuwa vizuri sana watueleze ni muda gani ama masaa mangapi ambayo hili neno “pole pole” litaanza kufanya kazi. Lakini sasa, hili ni neno tu lililowekwa pale. Tunataka kuwaambia akina mama katika nchi yetu ya Kenya kwamba tunataka kuwakumbusha ndugu zetu kuwa tumeenda shule, tumesoma na tunaelewa Kimombo. Kwa hivyo, hawawezi kutubabaisha na maneno kama hili neno ‘progressive.’ Tunalielewa kwa sababu tumeenda shule kama wao, tuna akili kama wao na, hata hapa, tunachangia vile wao wanachangia. Nataka kushukuru sana ile nafasi sisi akina mama tumepewa kufika katika Bunge hili letu. Tumejifunza mambo mengi tangu tuje. Hiyo miaka minne ambayo imepita, tumejifunza mengi. Sasa tuna namna vile tunaweza kumenyana na hawa ndugu zetu ikifika wakati wa kura pale maeneo ya uwakilishi Bungeni. Nataka kumhakikishia dadangu Mhe. Millie kutoka kule Mbita kwamba tunajua ni yeye tu ndiye Mbunge mwanamke ambaye amechaguliwa katika Bunge hili kwa chama chetu cha ODM. Sisi tunamhakikishia ya kwamba 2017 tutakuwa wengi hapa Bungeni kwa sababu tumepewa zile nguvu ambazo tunahitaji; tumefunzwa na pia tumejifunza wakati huu ambao tumekuwa hapa Bungeni. Nataka kuwaambia akina mama wote katika nchi hii yetu ya Kenya kwamba, sisi tumejifunza, tumeona dalili ya hili Bunge leo. Unaweza kuhesabu ni wanaume wangapi wako hapa. Leo hii wametuachia Bunge ili tuongee mambo ya akina mama. Tukizungumza mambo ya jinsia au ‘gender’ haimaanishi ni wanawake peke yao. Jinsia ni wanawake au wanaume. Kwa hivyo, nataka kuwaambia akina mama wa Kenya: Tafadhalini leo hii tunaelekea katika msimu wa kupiga kura. Tafadhali mkiona mama yeyote amejitokeza kusimama, huyo ndiye ningewaomba mmpigie kura ili tuweze kuangalia namna ya kuongezea namba za wanawake katika Bunge letu. Tunataka kuona magavana na maseneta wanawake wakichaguliwa. Tunataka kuona idadi ya Wabunge wanawake ikiongezeka. Nimepewa nguvu, najiweza na niko tayari kuingia katika eneo langu la Kakamega Kaunti. Nikiwa mzaliwa wa Khwisero, nitaenda kung’ang’ania kiti cha Ubunge pale Kwhisero ili nimpatie mama mwingine nafasi kufika hapa Bungeni kuongezea ile namba ya wanawake."
}