GET /api/v0.1/hansard/entries/702007/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702007,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702007/?format=api",
    "text_counter": 321,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Amolo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 631,
        "legal_name": "Rachel Ameso Amolo",
        "slug": "rachel-ameso-amolo"
    },
    "content": "Kwa hivyo, nawaambia akina mama pale nje: Tafadhalini, mwaunge mkono wale ambao tunawahitaji ili kuongezeka hapa Bungeni. Ukiangalia Wabunge akina mama ambao wamechaguliwa katika kaunti, kwa kweli, lilikuwa jambo gumu kabisa. Lakini ukiangalia utendakazi wao, wamefanya kazi kwa njia inayofaa kabisa. Ningewahimiza wale ambao wanaweza kung’ang’ania vile viti vya Ubunge, tafadhalini tokeni ili tuwapatie akina mama wengine nafasi kumenyana wapate viti hivyo. Leo hii, nafurahia sana kwa sababu wakati Rais Obama wa Marekani alikuja hapa, alisema jambo moja: Timu haiwezi kuwa timu kama haitachukua vijana na wanawake katika nchi. Haiwezi kuwa timu ya wanaume pekee ndio itacheza mpira. Kwa hivyo, tunahimiza The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}