GET /api/v0.1/hansard/entries/702008/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 702008,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702008/?format=api",
"text_counter": 322,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Amolo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 631,
"legal_name": "Rachel Ameso Amolo",
"slug": "rachel-ameso-amolo"
},
"content": "kwamba lazima hapa tuwe timu moja. Tuwe na vijana na akina mama ambao watacheza mpira pale kiwanjani. Na mpira unapochezwa, hakuna timu itakuwa na wachezaji 11 na wengine watano. Ikiwa timu zinachezesha watu 11, timu moja itakuwa na wachezaji 11 na ile timu nyingine pia itakuwa na 11. Sisi hatuulizi 11 kwa 11. Tunauliza tu kiasi ili akina mama waongezeke katika Bunge letu la Kenya. Leo hii ni jambo la ajabu sana kwa sababu siku zote tunapata Bunge limejaa ndugu zetu wanaume. Lakini leo akina mama, naliangalia Bunge na naomba Mwenyezi Mungu ahakikishe kwamba hapo mwaka wa 2017, viti hivi ambavyo viko wazi vijazwe na akina mama. Hii ni nafasi ambayo tunaona kwa kweli tukiwachiwa nafasi, tunaweza kufanya hii kazi. Ndio sababu ndugu zetu wametoka nje. Lakini sisi tunawaambia hivi vipasa sauti tunaweza kuvitumia vilivyo na nchi hii yetu ya Kenya bado itaendelea mbele. Kwa hivyo, nasema hii nafasi ni yetu na tukiendelea kuitumia, tutaweza kuongezeka ikifika mwaka wa 2017. Nawambia akina mama kule nje wampigie mama yeyote atakayesimama kuomba kura."
}