GET /api/v0.1/hansard/entries/702014/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 702014,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702014/?format=api",
"text_counter": 328,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Amollo",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 738,
"legal_name": "Rose Nyamunga Ogendo",
"slug": "rose-nyamunga-ogendo"
},
"content": "Ahsante sana, Mhe. Naibu Spika. Mhe. Savula ni Mbunge kutoka Kakamega Kaunti ninayemheshimu sana. Kama angeweza kunisikiliza vizuri, nimesema kwamba nawashukuru sana wale ambao wamebaki Bungeni kuunga Mswada huu mkono ama kuupinga. Hivyo ndivyo nilivyonena kwa lugha ya Kiswahili. Ningependa kumjulisha kwamba sikusema kwamba yeye ni mwanaume ama mwanamke. Tunao ufahamu kuwa yeye ni Mbunge wa Lugari na kwamba, yeye ni mwanaume. Tunamjua yeye kama Mhe. Savula. Sikusema vile anavyodhania. Namshukuru sana kwa kuwa katika kikao hiki cha leo. Ninampongeza zaidi. Naibu Spika, kwa hayo machache, ningependa akina mama wajitokeze. Wanaona vile tumebaki hapa wachache. Tunawaomba akina mama watuunge mkono tutakapojitokeza kule mashinani mwaka wa 2017. Kwa hayo machache, naupinga Mswada huu."
}