GET /api/v0.1/hansard/entries/702032/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702032,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702032/?format=api",
    "text_counter": 346,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Ahsante Mhe. Naibu Spika kwa kunipa nafasi hii nichangie mjadala huu wa jinsia ya kike. Nakubaliana na mnenaji, ndugu yangu Mheshimiwa aliyeongea kuhusu Mswada huu ulioletwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kisheria. Kama kiongozi katika Bunge hili, natumai wenzangu kule nje wananisikiliza ndiposa tuwaambie nini kinachoendelea. Jumamosi iliyopita, nilikuwa Bungoma kwa hafla ya mazishi mahali fulani. Mama mmoja aliamka akasema kwamba wale akina mama ambao wako Bungeni hawataki kushughulikia masuala ya akina mama kule nje. Alisema kwamba tuwe na akina mama wengi ndiposa sauti zetu zisikilizwe katika Bunge. Niliwahakikishia wananchi kwamba viongozi ambao tuko Bungeni, haswa akina mama, tutahakikisha kwamba masuala ya akina mama ama jinsia ya jamii moja yatashughulikiwa. Nimesikiliza wenzangu wakisema kwamba iwapo tutaongeza idadi ya akina mama katika Bunge, huenda Bajeti itakuwa juu na nchi yetu itagharamika sana. Wakati walipobuni Maeneo Bunge 290, hawakuangalia mambo ya bajeti. Lakini tukizingatia kuwa na akina mama katika Bunge, wanaongea kuhusu bajeti. Ningependa kumshukuru Mhe. Millie Odhiambo kwa kusema kuwa akina mama pia wanafaa kuja Bungeni na, vile vile, kuwakilisha nchi yetu katika nyadhifa mbalimbali. Ningependa kuwashukuru kwa sababu walihakikisha kuwa tuna akina mama 47 katika Bunge hili. Tumeshikana na wale wenzetu ambao walichaguliwa - ukiwa mmoja wao - kuhakikisha kuwa tunapigania masuala ya akina mama nchini. Ningependa kumshukuru Mhe. Rais kwa kumpendekeza Waziri Amina Mohamed kwa Muungano wa Afrika. Tungependa kuwaambia ndugu zetu wa kiume kuwa iwapo wanasema kuwa masuala haya yatatusaidia sisi kama akina mama na viongozi, basi lazima wafikirie pia ndugu au dada zao ambao wanaweza kuwa kwenye nafasi kama hizi zetu. Ningependa kumuunga mkono dadangu Nyokabi kuhusiana na suala la idadi ya wanawake katika Kamati zetu. Amesema kuwa Kamati yao ina wanawake watano tu, ilhali wanaume ni 25. Itakuwa vigumu sana kuzungumzia mambo ya jinsia moja katika Kamati zetu. Ningependa kumwambia Naibu Spika kwamba aende apiganie kiti cha ugavana katika eneo la Bomet. Ningependa pia kuwaambia Millie Odhiambo na Rachel Shebesh kuwa wasiogope kutafuta viti vya kisiasa kwa sababu tutawaambia akina mama wawachague. The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}