GET /api/v0.1/hansard/entries/702033/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702033,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702033/?format=api",
    "text_counter": 347,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Wanyama",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1076,
        "legal_name": "Janet Nangabo Wanyama",
        "slug": "janet-nangabo-wanyama"
    },
    "content": "Tumeelezwa kuwa kuna mtu ambaye alienda mahakama kutaka kujua kwa nini tumechelewa kutekeleza Katiba hii. Nimeshangaa sana kusikia wenzetu wakisema kuwa Katiba hii ni mbaya kwa asilimia 20. Kwa nini waliipitisha Katiba hiyo na makosa hayo bila kuangalia uongozi wa wanawake? Wanawake lazima wawe na nyadhifa mbalimbali katika nchi yetu. Ni lazima tuwatendee haki akina mama ambao ni viongozi nchini. Katika eneo langu, akina mama ambao ni viongozi ni wachache sana. Nilikuwa diwani, lakini sikubaki hapo kwa sababu nilihakikisha kuwa nimepigania kiti na nikachaguliwa kama mwakilishi wa akina mama katika kaunti. Tusilale bali tuhakikishe kuwa masuala yetu yanatekelezwa. Tukiwa kule nje, tunaweza kueleza wenzetu kuwa masuala yao yanawakilishwa vizuri hapa Bungeni. Napinga Mswada huu."
}