GET /api/v0.1/hansard/entries/702573/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702573,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702573/?format=api",
    "text_counter": 120,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Asante sana, Mhe. Spika. Nami pia ningependa kuunga mkono wenzangu wengi ambao wameongea kuhusu Mswada huu. Kutoka mwanzo, mimi niko hapa kupinga vikali sana Mswada huu ambao umeletwa na Mhe. Chepkong’a. Napinga Mswada huu kwa sababu umeletwa eti utekeleze matakwa ya Katiba. Wakati Katiba ilikuwa ikitengezwa, maoni yalitolewa na Wakenya wengi. Kwa wakati huo, tulisema kuwa “Wanjiku, Kadzo, Anyango, Chebet, Kibet na Onyango wameongea. Haikuwa ni maneno ya Wabunge zaidi ya 300 ambao tuko katika Bunge hili la taifa. Wakenya walifikiria kuwa hapo awali kulikuwa na dhuluma za kihistoria katika mambo ya uongozi. Tunajua akina mama wamenyanyaswa kwa misingi ya desturi zetu, tamaduni zetu na hata dini zingine ambazo zinasema kuwa kazi ya mama ni ya nyumbani kama vile kupika, kufua The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}