GET /api/v0.1/hansard/entries/702574/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 702574,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702574/?format=api",
"text_counter": 121,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": "na pengine kumstarehesha mzee. Kweli, tunakubali kwamba kuna zile kazi ambazo ni mwafaka kwa kina mama kuzifanya. Lakini wakati huu, nchi yetu, katika Riwaza 2030, ilizungumzia kuwa akina mama ni lazima wajenge uwezo kisiasa, kijamii na pia kiuchumi. Iwapo tutapitisha Mswada ambao unasema eti tutatekeleza sheria hii ya Katiba pole pole, pasina kutueleza kinaga ubaga njia mwafaka itakayotumika, watueleze ni kwa muda gani tutatekeleza na ni idadi ya asimilia ngapi ambayo itaweza kuwekwa kuhakikisha kwamba zaidi ya thuluthi mbili haitakuwa ya jinsia moja. Tunawapenda sana ndugu zangu Wabunge wanaume. Nataka niwaambie kwamba Mswada huu ni wa akina mama. Ni Mswada wa jinsia kumaanisha kwamba itafika wakati ambapo nyinyi pia mtahitaji kusaidika na Mswada huu. Kwa hivyo, unapochimba kisima, usije ukaingia wewe mwenyewe. Sura ya 27(8) inazungumzia kuwa Serikali iweke mikakati na sera zitakazohakikisha kwamba makundi ambayo yalikuwa yametengwa katika jamii, ambayo tunaita kwa Kiingereza,"
}