GET /api/v0.1/hansard/entries/702576/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 702576,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702576/?format=api",
"text_counter": 123,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 874,
"legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
"slug": "mishi-juma-khamisi"
},
"content": ", yatafikia uongozi na kuwa sawa na zile jinsia zote. Iwapo sisi ni wakweli kama watunzi wa sheria katika Jamhuri yetu ya Kenya, lazima tuweke sheria za ukweli. Tusiweke sheria tu ati kwa sababu tumesikia Bunge litavunjwa iwapo hatutaweka sheria hii. Mahakama Kuu, tunayoiita kwa Kiingereza Supreme Court, ilitupatia mawaidha na kusema tutengeneze sheria mwafaka itakayotupatia njia sahihi ya kueleweka na kuhakikisha kwamba sheria ambayo iko katika Sura 81 imetekelezwa. Kwa hivyo, tukisema tunapitisha Mswada huu, bado hatujafanya jambo lolote. Bado tutarudi nyumbani hivyo hivyo. Sasa tunasikia kuwa kuna kesi. Kama tutaendelea kwenda hivi, basi sisi tutakuwa mashakani sana kuweza kuhakikisha kuwa ukweli umepatikana. Tuna mifano mingi. Mhe. Rais alimteua Mama Amina Mohamed katika Wizara ya Mashauri ya Nchi za Nje. Leo hii, alijengeka uwezo mpaka sasa anataka kupigania kiti kikubwa katika Umoja wa Mataifa ya Africa nzima. Kama hangeteuliwa na kupewa kiti kama kile, angepata nguvu gani za kumwezesha kusimama? Mifano tunayo. Mhe. Cecily Mbarire kwanza aliteuliwa kisha akaweza kusimama na sasa atakwenda kupigania kiti cha ugavana. Hiyo ndio njia. Mimi mwenyewe nimechaguliwa kama mwakilishi wa akina mama. Nimepata nguvu, nimejenga uwezo na sasa nitapambana na yule Mbunge wa Eneo Bunge la Likoni. Najua nitaweza na nitakuja katika Bunge hili kama Mbunge wa Likoni. Kwa hivyo, ndugu zangu akina baba, hamuoni raha nyinyi tukiwa hapa Bunge tumekaa sako kwa bako, mama hapa na baba pale? Sasa hivi, mumeniona nimekaa hapa na Mhe. Bedzimba yupo karibu na mimi. Hata wakati anachangia, ana raha kwa sababu Waingereza walisema, “ unlike poles attract, like poles repel” . Haya si maneno ya kuzungumza tu ya sayansi. Ni lazima jinsia zikiwa pamoja, mambo huenda sambamba na tukaweza kujenga nchi yetu."
}