GET /api/v0.1/hansard/entries/702579/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702579,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702579/?format=api",
    "text_counter": 126,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "hatuelewi zitatekeleza vipi sheria ambazo zimezungumziwa katika sheria mama inayoitwa Katiba? Lazima tuangalie kule tunakotoka na kule tunakoenda. Leo hii tukisema hatutaweza kutekeleza sheria hii, kesho kutwa tutakuwa na Bunge ambalo lina akina mama kumi. Itakuwa ni aibu na fedheha. Lazima pia tuwe tunazingatia nyanja hizo. Leo wewe kama Mbunge mwanaume pengine umejaaliwa watoto wa kike pekee, lazima upitishe sheria ambazo haswa zinamlenga mtoto wa kike. Ijapokuwa ni jinsia, ukweli ni kwamba mama alikuwa amegandamizwa kihistoria, kidesturi, kimila na pia katika mambo ya kupigwa na mambo ya kiuchumi. Tulikuwa tumegandamizwa sana. Hatusemi kuwa sisi tunaomba lakini tunataka tuiweke Kenya yetu iwe inapendeza hata miongoni mwa yale mataifa mengine. Pia sisi kama Wakenya, tuna sheria kama ile mikataba ya kiulimwengu ambayo tumetia sahihi ya kwamba tutahakikisha haki za akina mama katika kisiasa, uchumi na jamii. Leo hii mambo haya yote tunayafahamu lakini tukirudi nyuma, tunamwangalia mwanamke kana kwamba ni chombo tu. Mjue akina mama kura tunazo na kura zetu ni nyingi. Tukiamua wakati huu kuwa dawa ya moto ni moto, naona wengine watapata shida hapa Bungeni. Maanake tutaongea na hatutanyamaza. Tutaongea kinaga ubaga kwa sababu nipe nikupe ndio biashara iliyoko sasa. Hakuna biashara nyingine. Biashara ni nipe nikupe. Hatutakuwa tunawasaidia. Hapa kulikuwa na Mswada wa mambo ya Hazina ya Kitaifa ya Maeneo Bunge na sisi kama Wawakilishi wa Akina Mama ambao hatuna hiyo Hazina tulisimama kidete tukaunga mkono kwa sababu sisi tuko pamoja na ni wapenzi, sako kwa bako, tusonge mbele kama Wakenya. Leo hii mbona nyinyi mwatubwaga? Itakuwa si sawa jamani. Palipo na wema lazima kurudi wema. Sisi tunapowafanyia wema lazima nanyi mregeshe wema. Kwa hivyo, mimi najua hatujachoka. Najua ndugu zangu viongozi wa kiume mnatupenda. Najua hata leo ukipinga Mswada huu na useme tutengeze Mswada mwafaka, hata ukifika nyumbani makaribisho yako yatakuwa tofauti."
}