GET /api/v0.1/hansard/entries/702582/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702582,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702582/?format=api",
    "text_counter": 129,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Khamisi",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 874,
        "legal_name": "Mishi Juma Khamisi",
        "slug": "mishi-juma-khamisi"
    },
    "content": "Akina mama tumejaribu sana. Dada yangu Rose Nyamunga amesema kuwa tuliwanunulia dinner . Lakini sisi hatutaki kuwadai. Ile ilikuwa ni mapenzi yetu. Natutaendelea kufanya mengi mazuri ili sisi tuwe kitu kimoja, tuwe na upendo na mapenzi jamani. Wenzetu hapa Tanzania, Makamu wa Rais wao ni mama. Hiyo ndiyo njia ambayo sisi tunastahili kuendelea nayo. Lakini hivi hivi bila kuwajenga kiuwezo akina mama, hatutafikia pale. Na kama tunataka kutajika katika ulimwengu kwa mambo ya uongozi, lazima tuhakikishe akina mama wako mbele, tumewasaidia na wamepata haki yao. Natukifanya hivyo, basi Kenya itakuwa miongoni mwa inchi ambazo zimestawi na kubobea kiuchumi, mambo ya kijamii na siasa."
}