GET /api/v0.1/hansard/entries/702628/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702628,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702628/?format=api",
    "text_counter": 175,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "Asante sana Mhe. Spika. Nami pia najiunga na wenzangu kupinga Mswada huu ambao unarekebisha Kipengele cha 81 cha Katiba. Si utani kuwa Kipengele cha 81 kiko pale, si utani kuwa Kipengele cha 27 kiko ndani ya Katiba haswa kwenye ukurasa wa masuala ya haki za kibinadamu. Hakuna uwezekano kuwa Wakenya wataweza kufanya shughuli za kimaendeleo na uongozi bila kuhusisha akina mama, walemavu ama wale ambao ni wanyonge katika jamii na ulimwenguni ili kupata suluhu kwa masuala mengi yanayowakabili Wakenya. La kusikitisha ni kwamba wengi wetu tumeongea mara kwa mara kuhusu jambo hili ambalo linahusu Wakenya wote na hata ulimwengu mzima. Ni suala ambao limeleta kero kwa wale wengi ambao wameachwa nje bila kuhusika kwenye masuala ya uongozi nchini. Mhe. Spika, ni wazi kwamba Katiba hii ambayo tulipata mwaka wa 2010 iliongeza idadi ya akina mama Bungeni. Haikuongeza idadi inavyotakikana lakini mabunge ya magatuzi yameweza kupata idadi ya akina mama inavyostahili. Katika Bunge la taifa na Bunge la Seneti, tunasikitika kuwa idadi ya jinsia moja haikufika theluthi moja ambayo imetajwa katika Katiba. Ninayosema si utani. Wakenya walifanya uamuzi. Wakati huo nilikuwa na wasiwasi sana kuwa hatukuweka kipengele cha kutuonyesha jinsi idadi hii itafikiwa. Niliona kama kungekuwa na tatizo. Ukweli ni kwamba tatizo hilo tunalo sasa. Tuna wasiwasi kuwa mahakama yetu huenda yakaamua kwamba Bunge hili halijaridhia haja za Katiba yetu. Wakati ule nilikataa kuafikiana na kielelezo cha Katiba kwa sababu nilifikiri tutapata matatizo makubwa kupata suluhu. Niliona ingekuwa vigumu kupata nafasi zaidi za wanyonge katika Bunge hili. Idadi ya akina mama Bungeni yafaa kuongezwa kwa sababu wananchi ndio walifanya uamuzi. Ninayo furaha kuwa sasa hivi, kuna akina mama 47 ambao wamekuja hapa kwa kupitia kipengele maalum ili waweze kuchukua viti ambavyo wao wenyewe wanapigania katika kusimamia uongozi. La kusikitisha ni kuwa, bado, Wakenya hawajaamua kuchagua akina mama wa kutosha. Kwa sababu ya The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}