GET /api/v0.1/hansard/entries/702629/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702629,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702629/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Dr.) Shaban",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 139,
        "legal_name": "Naomi Namsi Shaban",
        "slug": "naomi-shaban"
    },
    "content": "masikitiko hayo niliyonayo, ninawaomba ndugu zangu katika Bunge hili tushikane mikono pamoja ili tutafute suluhisho la tatizo hili. Mswada huu ulioko mbele yetu sasa hivi hautupatii suluhisho bali unatuweka kwenye matatizo. Mswada huu unanuia kwamba tatizo hili lishughulikiwe siku za baadaye. Hakuna Bunge lingine ambalo lingeweza kutatua tatizo hili. Hii ni kwa sababu Bunge hili, hivi maajuzi, karibu lipitishe idadi inayostahili ya theluthi moja tunayoulizia kikatiba. Theluthi moja siyo kubwa sana. Hivyo basi, ninatumaini kuwa Mswada huu, kama tutakubaliana, uwekwe kando ili tuweze kupata Mswada wa kuleta sheria ambayo itatupatia suluhisho na idadi iweze kutimia. Hata kama tutakubaliana kusonga mbele pole pole, basi Mswada huu usongezwe mbele baada ya sisi kupitisha idadi jinsi inavyotakikana katika Katiba. Haijalishi hata kama itakuwa ni asilimia 30 au 40. Hivyo, tutakuwa tunakaribia kufikia kiwango hicho. Lakini kwa sasa hivi, tukiacha mambo yabaki yalivyo, itakuwa kama kwamba tunafunga mlango. Sisi hatutakubaliana kama Bunge la 11 kuwa hii ni sawa. Walemavu bado wako nje. Idadi yao haijatimia. Aidha idadi ya vijana haijatimia. Ninapinga Mswada huu nikiwaomba ndugu zangu, haswa, wale wa jinsia ya kiume, tushikane pamoja tuweze kutekeleza suala hili na kupata suluhisho bila sisi kukosana. Sisi ni watu wa umoja na tuko Bunge la 11 siyo tu kwa bahati na sibu. Wananchi walituchagua na kutupatia nafasi hii ya kuwawakilisha katika Bunge hili. Naomba kupinga Mswada huu."
}