GET /api/v0.1/hansard/entries/70268/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 70268,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/70268/?format=api",
    "text_counter": 268,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Mr. Kutuny",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 61,
        "legal_name": "Joshua Serem Kutuny",
        "slug": "joshua-kutuny"
    },
    "content": "Bw. Naibu wa Spika, nitauliza swali langu kwa lugha rahisi ili kila mtu aielewe. Je, ni ukweli kulikuwa na mkataba kati ya Bw. Ocampo, Waziri Mkuu na Rais? Je, ni ukweli mkataba huu ulishurutisha Serikali isiingilie kati wakati korti la kimataifa litawakamata washukiwa hawa sita na kuwa wao hawatakuwa vizuizi na watakuwa tayari kuwashika washukiwa hawa? Inasemekana kulikuwa na mvutano kati yenu wawili. Waziri Mkuu alikuwa tayari kutia sahihi yake katika mkataba huo lakini Rais alikataa katakata kutia sahihi na kusema sheria ifuate mkondo wake. Je, mkataba huu ulinyima Serikali mamlaka yoyote juu ya washukiwa hawa? Ninataka Waziri Mkuu athibitishe madai hayo."
}