GET /api/v0.1/hansard/entries/702711/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702711,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702711/?format=api",
    "text_counter": 258,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Korere",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 13134,
        "legal_name": "Sara Paulata Korere",
        "slug": "sara-paulata-korere"
    },
    "content": "Ahsante Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuongeza sauti yangu katika kuupinga Mswada huu ambao umewasilishwa hapa na Mhe. Chepkong’a. Inafaa ifahamike kwamba Katiba hii inayowapatia akina mama nafasi zaidi katika Bunge haikupitishwa na akina mama peke yao, bali ilipitishwa na wananchi wa nchi tukufu ya Kenya. Iwapo Katiba itatupatia kwa mkono wa kulia na Bunge itunyang’anye kwa mkono wa kushoto, itakuwa aibu, fedheha na dhuluma. Sisi kama akina mama ambao tumehesabika katika Bunge hili la kumi na moja, tutaingia katika vitabu vya historia kama akina mama waliohudumu katika Bunge ambalo lilinyanyasa na kudhulumu akina mama. Mimi nikiwa Mbunge kutoka Laikipia, nimeingia Bunge hili kupitia uteuzi. Iwapo nisingepata fursa ya kuingia katika Bunge hili, nisingekuwa nazungumzia maneno ya kugombea kiti cha ubunge cha Laikipia Kaskazini mwaka wa 2017. Tunasema kwamba mtoto akizaliwa ni sharti umpe chakula ili akue. Jinsi akina mama waliwezeshwa kuingia humu Bungeni ni njia mojawapo ya kutayarisha miundo misingi ili kukuza maazimio yao ya kugombea viti na kuhesabika katika uongozi wa nchi hii tukufu ya Kenya. Mswada ambao umeletwa na Mhe. Chepkong’a unaturudisha nyuma. Mswada huo unadhulumu na kunajisi Kenya. Sote tunajua kunajisi ni kitendo chafu. Ni dhambi na hata hakitajiki. Hatuwezi kukubali Mswada ambao unanajisi Katiba ya Kenya ambayo sisi wenyewe tulipigia kura na ikawa sheria kuu inayoongoza nchi hii. Mwisho, ningependa kusema kwamba mimi ninakienzi chama cha Jubilee. Ninajivunia kuwa mmoja wa wanajubilee. Nakienzi kwa sababu hii: Ni chama ambacho kimesifika na kina umaarufu wa kutetea haki za wanawake. Chama hiki kinawatambua akina mama na kuwaheshimu. Ifikapo hiyo 2017, ninataka kuwarai wanawake wa Kenya nzima wasije wakauliza chama ni gani. Waangalie chama kinachoheshimu na kutetea akina mama. Katika upande ule wa Upinzani wa ODM, tumemwona mama mmoja peke yake ambaye ni Millie Odhiambo, ambaye amechaguliwa katika Eneo Bunge la Mbita. Yeye hupigwa vita kila mara. Hata tunapozungumza hapa--- Mimi si mwanachama wa ODM lakini ninajua Mhe. Millie Odhiambo anapigwa vita na wale mabwanyenye ambao wanajiita vigogo wa ODM. Kwa hivyo, ninawarai akina mama wavuke na kuungana na chama cha Jubilee ili tulete akina mama hapa Bungeni na tupunguze mzigo aliobeba punda ambaye wanasema amechoka. Tuchague akina mama, mimi nikiwa mmoja wao, kutoka idadi ya 60 kuendelea. Ninapinga."
}