GET /api/v0.1/hansard/entries/702716/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept
{
"id": 702716,
"url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702716/?format=api",
"text_counter": 263,
"type": "speech",
"speaker_name": "Hon. (Ms.) Chidzuga",
"speaker_title": "",
"speaker": {
"id": 751,
"legal_name": "Zainab Kalekye Chidzuga",
"slug": "zainab-kalekye-chidzuga"
},
"content": "Shukrani Mhe. Naibu Spika wa Muda. Ninachukua fursa hii kuupinga huu Mswada wa rafiki yangu Chepkong’a . Kwanza ninatoa mwito kwa wananchi wa Kenya nikianza na vijana, walemavu na akina mama, Mswada huu siyo wa mwanamke bali ni wa kutuweka katika hali ya usawa wa kijinsia. Leo ni sisi akina mama ndio tunalia, kesho itakuwa wanaume, kesho kutwa vijana na walemavu. Kwa hivyo, akina mama wa Kenya wanalilia Mswada huu kwa sababu mama ndiye mzazi wa kila mtu. Mhe. Chepkong’a na timu yake wanafaa waelewe kwamba ni huyu mama, kijana na mlemavu ndio wamewafanya wachaguliwe kuja hapa Bunge. Walemavu, akina mama na vijana wanastahili kupewa nafasi zao kamili ndani ya hili Bunge kama ambavyo Katiba inatarajia. Hili si jambo tunataka eti kwa ajili ya ubinafsi. Ni wanaume hawa walioketi katika Bunge lililopita na kugawanya maeneo bunge. Walijiongezea maeneo bunge. Ni wao waliwatwika mzigo mkubwa wananchi wa Kenya. Kama kweli wao wanazungumzia mzigo, tunataka tuwaone wakijitokeza waseme: “Ninatoa eneo langu la uwakilishi Bungeni liunganishwe na lingine ili tutoe nafasi ili Bunge lipunguze uzito.” Ni Wabunge hawa hawa wa kiume ambao wamelemaza uchumi wa nchi ya Kenya maana wao ndio wengi hapa. Sisi ni wachache. Ni Wabunge hawa hawa waliopiga kura katika mpangilio wa Bunge wakanyima wawakilishi wa akina mama pesa ya kutosha sawa na National Government Constituencies Development Fund (NG-CDF). Tukapewa chache, wakachukua nyingi. Mbona hamkusema kwamba sisi pia tuongezewe pesa tuwe sawa nanyi? Inamaanisha kwamba Waheshimiwa wenzetu wa kiume hawako tayari kuondoa mzigo kwa mwananchi wa Kenya. Wakati ni huu. Tukaeni tuzungumze tutoke kortini tuwe na uwiano. Tuondoe maeneo ya Bunge mengine, turejeshe yale ya zamani."
}