GET /api/v0.1/hansard/entries/702732/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702732,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702732/?format=api",
    "text_counter": 279,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Changorok",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1149,
        "legal_name": "Regina Nyeris Changorok",
        "slug": "regina-nyeris-changorok"
    },
    "content": "Ahsante sana, Bi. Naibu Spika wa Muda. Ningependa kuchukua nafasi hii kusema kwamba utovu wa usalama nchini Kenya umekuwa jambo la kuhuzunisha. Umeumiza watu wengi katika jamii nyingi. Hivi tunavyozungumza, tumepoteza watu wengi kwenye visa vya wizi wa mifugo, hali ambayo imesababisha kudorora kwa usalama katika nchi hii. Tunapozungumzia Kerio Valley, na haswa maeneo ya Tot, Marakwet, Pokot, Tiaty na Pokot Magharibi, tunafaa kufahamu kwamba haya ni maeneo ambako usalama umedorora. Nimeishi katika sehemu hiyo, na ninaelewa jinsi hali vilivyo. Kuuawa kwa watu kiholelaholela ni jambo la kuhuzunisha sana. Kifo ni tukio la kawaida. Kifo kinapowatembelea kulingana na mpango wa Mwenyezi Mungu, hatuna uwezo; lakini kifo kinachosababishwa na binadamu wenzetu kwa sababu ya kuzorota kwa usalama huwaumiza waathiriwa zaidi. Watu wengi nchini Kenya wamepoteza maisha yao kwa sababu ya kutokuwepo kwa ulinzi wa kutosha. Kwa mfano, jana watu wengi walipoteza maisha yao mjini Mandera. Hili ni jambo la kuhuzunisha sana. Ni jambo ambalo linafaa kutusukuma tuchukue hatua ya dharura. Ukosefu wa usalama nchini humu ni jambo ambalo linafaa kuzungumziwa. Hatufai kuketi chini tukiangalia tu huku watu wetu wakiuawa. Jambo hili pia linasababisha watoto wetu kuacha kwenda shuleni. Kuhusu mzozo unaoendelea kati ya jamii zinazoisih katika sehemu za Marakwet Magharibi na Baringo, tumezungumzia jambo hili kwa muda mrefu. Ni lazima tuchukue hatua kwa sababu wakazi katika Kaunti hizo mbili ni Wakenya. Mimi ni mkaaji wa Chesegon. Kwa muda mrefu sasa akina mama wamekuwa wakijifungua wakitembea, na kwa sababu hiyo tumepoteza watoto wengi. Tunaishi nje ya nyumba zetu kwa sababu ya kudorora kwa usalama. Tumepoteza watoto wengi kutokana na magonjwa yanayosababishwa na baridi. Huu ni msimu wa mitihani ya kitaifa ya Kidato cha Nne na Darasa la Nane. Watahiniwa katika shule kama vile Chesegon, Tot na Liter watafanya mtihani namna gani kama usalama The electronic version of the Official Hansard Report is for information purposesonly. A certified version of this Report can be obtained from the Hansard Editor."
}