GET /api/v0.1/hansard/entries/702733/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 702733,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/702733/?format=api",
    "text_counter": 280,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Hon. (Ms.) Changorok",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 1149,
        "legal_name": "Regina Nyeris Changorok",
        "slug": "regina-nyeris-changorok"
    },
    "content": "haupo? Matokeo ya mitihani ya wanafunzi katika shule za Tot na Chesegon yatalinganishwaje na matokeo ya mitihani ya wanafunzi katika sehemu nyingine humu nchini? Hakuna atakayekumbuka kwamba watoto wengine walifanya mitihani kwenye mazingira ambayo hayakuwa na usalama. Matokeo ya mitihani ya watoto kote yatasawazishwa kutumia vigezo sawia bila ya kujali kwamba watoto wengine waliathirika kwa sababu ya kukosekana kwa usalama. Tunaomba usalama uimarishwe katika sehemu hizo kwa sababu wakazi hawana utulivu ama usalama. Hatuwezi kukosa suluhu. Ninaamini ya kwamba tuna uwezo wa kumaliza shida hiyo. Watu wengi wameuchangia mjadala huu, wakiwemo wakazi wa sehemu hizo wenyewe. Kwa hivyo tunaomba sheria ichukue mkondo wake. Ningependa maafisa wa polisi na wananchi katika sehemu hizo washirikiane ili waweze kuleta suluhu kwa jambo hili."
}