GET /api/v0.1/hansard/entries/703052/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 703052,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/703052/?format=api",
    "text_counter": 267,
    "type": "speech",
    "speaker_name": "Sen. Madzayo",
    "speaker_title": "",
    "speaker": {
        "id": 679,
        "legal_name": "Stewart Mwachiru Shadrack Madzayo",
        "slug": "stewart-mwachiru-shadrack-madzayo"
    },
    "content": "Asante sana, Bw. Naibu Spika. Ni jambo la kusikitisha sana kumwona Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo akisema kwamba hakuna lolote linaweza kufanyika. Anatupa mikono yake juu ya hewa akisema sasa ile hasara ambayo wakulima wamepata hakuna lolote linaweza kufanyika. Anawashauri waende kortini kutafuta marupurupu yao ilhali korti si suluhisho. Wakulima wanataka kujua kama ile benki imefungwa ni hatua gani imechukuliwa hivi sasa. Kuona wale wakurugenzi wa hiyo kampuni wanatembea kwa barabara wakistarehe na huku wakulima ambao walifanya bidii na mikono yao kuyakuza mazao hayo wakiishi kama masikini ama walala hoi na hakuna kitu kinaweza kufanyika. Ni hatua gani Serikali itachukua kuona ya kwamba wakulima wa Kirinyaga na kwingineko nchini hawateseki kutokana na kuporomoka kwa benki hizi ambako pesa zilihifadhiwa? Ni hatua gani zinaweza kuchukuliwa kuweza kuwafanya wale wakurugenzi wa zile kampuni - ambao ni Wakenya na wanaishi hapa ndani ya hii nchi - kuwalipa fidia wakulima hawa?"
}