GET /api/v0.1/hansard/entries/704909/?format=api
HTTP 200 OK
Allow: GET, PUT, PATCH, DELETE, HEAD, OPTIONS
Content-Type: application/json
Vary: Accept

{
    "id": 704909,
    "url": "https://info.mzalendo.com/api/v0.1/hansard/entries/704909/?format=api",
    "text_counter": 176,
    "type": "other",
    "speaker_name": "",
    "speaker_title": "",
    "speaker": null,
    "content": "ni urembo tu lakini hakuna jawabu lolote ambalo tumelipata kutoka kwa Mwenyekiti. Mimi nimeihakiki katika ukurasa wa nne. Mimi nimenakili katika ukurusa wa nne unaosema kwamba Serikali imepeleka magari ya maji, kudunga mifugo sindano na kupeana vyakula. Bw. Spika wa Muda, ukienda Kilifi, utajua kwamba mambo sivyo yalivyo katika hii taarifa hii. Ni sharti wale wanaohusika na mambo kama haya waeleze vyema walivyotumia pesa hizo. Sisi ambao ni wakaazi wa Kilifi hatujaona vitu kama hivi. Jumamosi iliyopita nilipeleka chakula kule. Katika shughuli hiyo ya ugawaji wa chakula, sikuona hata gari moja ambalo lilileta msaada wowote. Katika ukurasa wa tano, inasemekana kwamba vitu kadha vimefanywa mwaka huu na hazina ya kukabiliana na ukame. Kufikia hivi, sasa utumiaji wa pesa hizo ambazo ni Kshs19 milioni hauko kwenye hesabu za Kilifi. Sijui Mwenyeketi ataweza kutueleza vipi kuhusu jambo hilo. Vile vile, kuna---"
}